Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Kapala Chakupewa Makelele akifungua
mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika jana wilayani hapo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya,Charles Mwakalila akisoma
ajenda za Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya
Chunya.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Chunya, Sosthenes Mayoka, akitoa salamu za Serikali
kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro kwenye mkutano
wa baraza la madiwani wa Chunya.
Madiwani na wakuu wa idara wakifuatilia kwa makini Mkutano wa baraza la Madiwani wa Wilaya ya Chunya uliofanyika jana.
KATIKA kuhakikisha gonjwa la
Ukimwi halisambai kwa kasi miongoni mwa Wananchi, Madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wameitaka Serikali kuongeza Kondomu katika maeneo
ya mikusanyiko.
Madiwani hao walitoa rai hiyo
katika Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika jana katika ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya hiyo, ambapo walisema katika maeneo ya Mfwenkenya, Lupa
na Namsinde yana kiwango kikubwa cha maambukizi.
Walisema ili kunusuru hali hiyo
ni bora Kondomu zikasambazwa za kutosha katika maeneo hayo ama kuwaruhusu
wafanyabiashara kuuza kwa wingi katika maduka yao ikiwa ni pamoja na kutoa
elimu jinsi ya kutumia na kujikinga na maambukizi.
Waliongeza kuwa maeneo ya ya
mikusanyiko ya watu ndiyo inatakiwa kupewa vipaumbele sana kutokana na kuwepo
mchanganyiko wa watu wenye tabia tofauti pamoja na mabinti wanaofanya biashara
za ngono.
Diwani wa kata ya Mbangara,
Abrahamu Sambira, alisema hali ya maambukizi inatisha kutokana na mabinti
kulazimisha kufanya ngono na wanaume kwa malipo ambapo hufikia hatua ya kuomba
hata mahindi kwa mwanaume asiyekuwa na fedha.
“ Ndugu zangu hali ni mbaya
mabinti wanalazimisha mapenzi ambapo wanakuuliza kuwa kama huna fedha lete hata
mahindi hivyo kuifanya shughuli hiyo kama halali wakati ni hatari” alisisitiza
Diwani huyo.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa
Wilaya ya Chunya, Dk. Sichalwe alisema suala la upatikanaji wa Kondomu ni kubwa
kwa Wilaya nzima hivyo ataendelea kulifanyia kazi ili kunusuru hali hiyo.
0 comments:
Post a Comment