Thursday, 21 August 2014

Alama ya ulaji ndizi yamponza Tavecchio

Carlo Tavecchio raisi wa shirikishoa la soka Italia ,lawamani
Shirikisho linalo simamia mpira wa soka ulaya,UEFA linania ya kumchunguza rais wa soka aliyechaguliwa wa shirikisho la soka huko Italia Carlo Tavecchio .
Tavecchino anashutumiwa pia kushukiwa alionesha ishara ya ubaguzi wa rangi wakati wa harakati za kampeni zake.
Kutokana na madai hayo, Tavecchio amekwisha omba radhi kwa kitendo hicho cha ishara ya kula ndizi, kitendo kinachojulikana kimataifa katika soka kama ishara ya ubaguzi wa rangi.
Hata hivyo msamaha wake umegonga mwamba na kushindwa kuzuia harakati zinazo endelea ,dhidi ya nafasi yake ya urais na hivyo kujitia kikaangoni,je atajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe? Ama atachomoka kwenye fitina hii? Tusubiri uchunguzi .

0 comments: