Arsenal hawana mipango ya kusajili mshambuliaji mwingine kuziba pengo la Olivier Giroud - hata kama vipimo vitaonesha ana jeraha kubwa.
Klabu hiyo haina nia ya kusajili mchezaji yeyote wa ushambuliaji kwa mkataba wa kudumu katika dirisha hili la usajili. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema atatazama kilichopo katika soko la wachezaji wanaopatikana kwa mkopo.
Wenger anapanga kuwategemea Alexis Sanchez, Joel Campbell, Yaya Sanogo, Lukas Podolski na Theo Walcott. Giroud alikuwa anapanga kukutana na mtaalam ili kutathmini athari ya jerha lake, alilopata katika mchezo dhidi ya Everton siku ya Jumamosi uliomalizika kwa sare ya 2-2.
Kuna wasiwasi kuwa huenda amevinjika kiwiko cha mguu na huenda akakosa kucheza kwa karibu miezi mitatu.
0 comments:
Post a Comment