Thursday, 28 August 2014

BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LIMEFUNGULIWA LEO DAR ES SALAAM

1 
Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) la kwanza kufanyika Dar es Salaam, tangu utaratibu wa kufanyika kwa bunge hilo kwa mzunguko kwa kila nchi mwanachama wa Jumuiya.
2 
Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa akizungumza kwenye ufunguzi wa bunge hilo. 3 
Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda (kushoto) akiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa wakati wa ufunguzi wa vikao vya bunge hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo 4 
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Abdullah Juma Saadala (wa pili kushoto), akifuatilia ufunguzi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Phyllis Kandie  (Waziri kutoka Kenya) Shem Bagaine (Waziri kutoka Uganda), Leontine Nzeyimana (Waziri kutoka Burundi), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Jumuiya hiyo Wilbert Kaahwa 6 
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Jumaa Saadala akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam 7 
Wabunge wa Tanzania wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia hutuba ya Spika wa bunge hilo (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

0 comments: