Taarifa katika tovuti ya TFF imesema kwamba hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo juzi.
Kwa
muda sasa, kumekuwa na tuhuma nyingi za wachezaji na marefa kuhongwa
ili kupanga matokeo- lakini hakukuwa na sheria madhubuti ya kupambana na
hali hiyo- lakini kwa hatua hii mpya ya TFF dhahiri itasaidia kupunguza
mchezo huo mchafu.
Aidha,
baada ya Libya kujitoa kuwa mwenyeji wa Fainali za Afrika (AFCON) za
2017, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limealika nchi wanachama kuomba
uenyeji wa fainali hizo.
Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Agosti 24, mwaka huu imeamua Tanzania kuomba uenyeji wa fainali hizo.
“Tunatambua
kuwa moja ya masharti ya kuandaa fainali hizo ni pamoja na nchi kuwa
imeandaa moja ya mashindano ya vijana. Lakini kwa kuwa suala hili liko
katika mazingira maalumu (exceptional circumstances) tunaamini CAF
watafikiria ombi letu kwa msingi huo,”.
Awali
Libya ilipewa uenyeji wa fainali hizo 2015, lakini zikahamishiwa Afrika
Kusini kutokana na sababu za kiusalama. Hivyo, Libya ikapewa fainali za
2017 ambapo sasa imejitoa yenyewe kuandaa fainali hizo.
Wakati
huo huo: Kamati ya Utendaji ya TFF imemteua Boniface Wambura kuwa
Mkurugenzi mpya wa Mashindano kuanzia Septemba 1 mwaka huu.
Kabla
ya uteuzi huo, Wambura alikuwa Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF
kuanzia Januari 1, 2011. Nafasi hiyo sasa iko wazi na itajazwa baadaye
na Kamati ya Utendaji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya TFF, Geoffrey Nyange 'Kaburu' |
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
0 comments:
Post a Comment