Idara
ya Uhamiaji Nchini, imewakamata Raia wa nane (8) wa kigeni wakati
wakiingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere,
wakiwa na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya Ulaya.
Wageni hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini tarehe 15.08.2014 majira
ya saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la Ndege la Uturuki yenye
Namba TK 603, wakitokea Uturuki na kujitambulisha kuwa Raia wa Sweden
na Belgium.
Maofisa Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na
kuwafanyia ukaguzi wa kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq
wakijaribu kuingia nchini Tanzania na pasipoti za bandia.
kukamatwa
kwa wageni hao ni jitihada za Idara ya Uhamiaji kupambana na Uhamiaji
haramu nchini ambapo suala la Udhibiti wa Mipaka linapewa kipaumbele.
akizungumzia tukio hilo, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tatu
Burhan, anasema, kwa kutumia ujuzi na weledi walionao Maofisa Uhamiaji
wanaendelea kufanyakazi usiku na mchana kuhakikisha Sheria
na Taratibu za Uhamiaji zinafuatwa. "Idara ya Uhamiaji, iko macho
hatulali kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa nchi ikiwa ndio jukumu letu
namba moja unaimarika. kwahivyo, kila mtu awe Raia wa kigeni na
Watanzania wanapaswa kufuata Sheria na Taratibu zilizopo za kuingia na
kutoka nchini" .
Hadi sasa, Wageni hao wamezuiliwa kuingia nchini na wanaendelea
kushikiliwa na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji kituoni hapo huku wakisubiri
kurudishwa walikotoka. Hili ni wimbi lililoibuka hivi karibuni kwa
baadhi ya Raia wa nchi za Iraq, Iran, Syria kujaribu kuingia nchini
isivyo halali huku ikisemekana lengo lao kubwa ni kuingia Tanzania na
baadae kutoka kuelekea Mataifa ya Ulaya.
Majina
ya Wageni hao na Pasipoti bandia walizokuwa wakitumia pamoja na Majina
halisi na Pasipoti zao za Iraq zilizogunduliwa baada ya upekuzi kwenye
mabano ni kama ifuatavyo;
1. ADEL SHAALAN MOHAN - SWEDISH, PPT. NO. EI282207 ( ADEL SHAALAN MOHAN Pasipoti Nam. G1489664)
2. SAMER HELMI KAMIT - SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA HITEET, PPT. Namba, A 13466001)
3. MOHAMMED JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)
4. DAVID GABRIEL POBLETE - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT NO. A 4910203)
5. SADDAM ALKHAMERI AREF - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN, PPT. NO. G 1489664)
6. ALI MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725
7. OSAMAH ZAID GHAEB AL-OBAIDI - IRAQ, PPT. NO. A 6175951
8. ALI HUSSEIN OLEIWI - IRAQ, PPT. NO. G 1111623
0 comments:
Post a Comment