DODOMA
JUKWAA la katiba nchini
limeshauri,mchakato wa kuandika katiba mpya uahirishwe hadi baada ya uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015 kutokana na jukwaa hilo kudai kuwa yapo mambo mengi yanayokwamisha
mchakato huo.
Akizungumza na waandishi
wa habari mjini Dodoma mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deus Kibamba,ameyataja
baadhi ya mambo hayo kuwa ni mahudhurio hafifu ya wajumbe wa bunge hilo hivyo
kushindwa kushirikiana vema katika kuandaa mchakato huo.
Amesema kuwa mbali na
hilo kuwepo kwa michakato mingine mikubwa kama unadikishaji unaoendelea wa
vitambulisho vya taifa ,uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa
njia ya kielektroniki na uchaguzi wa Serikali za mitaa haiwezi kwenda sambamba
na mchakato wa katiba mpya bila kuathiri kiwango cha ushiriki wa wananchi na
ubora wa katiba itakayopatikana.
Aidha Kibamba amefafanua
kuwa utungaji wa katiba mpya unahitaji miaka ipatayo miwili tangu kupitishwa
kwa katiba mpya hadi kukamilisha uandaaji na upitishaji wa sheria zote
takriban 50 zinazohitajika ili kusaidia utekelezaji wa katiba mpya .
Hata hivyo Kibamba
ameongeza kuwa kitendo cha wajumbe kutoka kundi la UKAWA kugawanyika na hata
baadhi ya wajumbe kutoka CCM kutofautiana kauli katika mchakato huu inaonesha
kuwa taifa limeanza kugawanyika na utatuzi pekee ni kusitisha mchakato wa bunge
maalumu la katiba.
0 comments:
Post a Comment