DURU za habari zinaeleza
kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzaniam Taifa stars, Mholanzi, Mart Nooij
amemuondoa winga machachari wa timu hiyo na klabu ya Yanga, Mrisho Khalfan
Ngassa `Anko` katika kikosi kitakachopepetana na Msumbiji `Black Mambas`.
Imeelezwa kuwa Nooij
amefikia maamuzi hayo baada ya Ngassa kushindwa kuripoti katika kikosi chake
siku kilipojipima ubavu dhidi ya Botswana na kulala mabao 4-2, mjini Gaborone.
Kabla ya mechi hiyo, kocha
Nooij alimuita Ngassa, lakini alikaidi na kwenda Bondeni, Afrika kusini kufanya
majaribio na klabu inayoshiriki ligi ya huko, Free State Stars ambako alifuzu,
lakini uhamisho umekuwa mgumu.
Ngassa baada ya kufuzu
majaribio, klabu ya Free state ilitangaza kutuma ofa ya dola elfu 80 sawa na
milioni 130 za Kitanzania, lakini inasemekana Yanga waligoma.
Hata hivyo uongozi wa Yanga kupitia kwa katibu mkuu, Beno Njovu alisema kuwa Free State hawajafika mezani kuzungumza nao bali wanasikia kwenye vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment