..JE, ATAONDOKA ATLETICO MADRID?
Diego Simeone anaweza kuondoka Atletico Madrid majira ya kiangazi mwaka huu, huku akiwavutia watu wengi.
DIEGO Simeone ndiye kocha aliye kwenye
moto kwasasa na anaongoza kupigiwa upatu wa kutwaa kazi ya ukocha mkuu
wa timu ya taifa ya Hispania kama Vicente del Bosque anaachia au kama
kocha wa Argentina, Alejandro Sabella atashindwa katika mechi ya robo
fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ubelgiji.
Simeone mwenye miaka 44 ameingia
katika orodha ya makocha wanaosakwa sana baada ya kuonesha kiwango cha
juu akiwa na Atletico Madrid ambapo alitwaa ubingwa wa La Liga na
alifika fainali ya UEFA.
Muargentina huyo anaweza kwenda
kuiongoza nchi yake, lakini taarifa kutoka vyanzo vya karibu na Simeone
vinasema kuwa ana matarajio makubwa ya kuiongoza Hispania.
Simeone anaweza kumfundisha Messi na Argentina wakati huu hatima ya baadaye ya Alejandro Sabella ikiwa mashakani.
Kocha mpya? Hispania wameanza mipango ya kutafuta mrithi wa Vicente Del Bosque.
Maamuzi ya hatima ya Del Bosque
yameshafikiwa na kuteuliwa kwa Simeone kutamfanya kuwa kocha wa kwanza
wa kigeni kuifundisha Hispania kwa zaidi ya nusu karne.
0 comments:
Post a Comment