Anatua katalunya: Barcelona wana matumaini kukamilisha usajili wa Suarez kutoka Liverpool wiki hii.
BARCELONA wanatarajia kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez ndani ya saa 48 zijazo.
Mazungumzo
yanaendelea na miamba hiyo ya Hispania inataka kulipa moja kwa moja
dau waliloambiwa juu ya nyota huyo mwenye miaka 27. Liverpool wanahitaji
paundi milioni 80.
Licha
ya kufungiwa miezi minne kucheza soka kwa kosa la kung`ata, Suarez
ataruhusiwa kuchukua vipimo vya afya na tayari kamati ya nidhamu ya FIFA
imethibitisha.
Majanga: Suarez amefungiwa miezi minne baada ya kumng`ata beki wa Italia Giorgio Chiellini.
Mshambuliaji huyu wa Liverpool amefungiwa kujihusisha na shughuli zote za soka ikiwemo uwanjani, lakini haitamzuia kuhama klabu kama dili limekubaliwa
Mkuu wa kamati ya nidhamu ya
FIFA, Claudio Sulser, alisema: "Mchezaji hawezi kufanya shughuli yoyote
inayohusu mpira wa miguu, lakini vipimo vya afya kwa ajili ya uhamisho
jibu ni ndiyo. Kifungo hakiingiliani na haki za uhamisho"
Suarez alikata rufaa dhidi ya kifungo
chake cha miezi minne kwa kitendo chake cha kumng`ata mchezaji wa
Italia, Giorgio Chiellini.
Akiwa kazini: Suarez amekata rufaa kupinga adhabu ya kifungo cha miezi minne.
Kikao cha jumatano baina ya klabu mbili kilienda vizuri na kuna matarajio makubwa ya kufikia makubaliano.
Mkurugenzi mkuu wa Liverpool, Ian Ayre alikutana na maofisa wa Barca Raúl Sanllehí, Toni Rossich na Jordi Mestre.
0 comments:
Post a Comment