
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba sc, Zacharia Hans Poppe
MWENYEKITI wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba,
Zacharia Hans Poppe ataendeleza kuiongoza kamati hiyo katika uongozi mpya
ulioingia madarakani juni 29 mwaka huu.
Rais mpya wa Simba sc, Evans Elieza Aveva ametangaza
kumteua Poppe kuendelea kuwa mwenyekiti, huku Kassim Mohammed Dewji akiteuliwa
kuwa makamu mwenyekiti.
Aveva pia amewateua wajumbe wa kamati hiyo ya
usajili ambao ni Said Tuliy, Musley Al Ruwaih, Crescentius Magori na Dk Roadney
Chiduo.
Rais Aveva pia ameunda kamati mbili, moja ya soka
la vijana na kamati ya mashindano.
Kamati ya soka la vijana itakuwa chini ya
mwenyekiti wake Said Tully. Wajumbe wengine ni Ally Suru, Patrick Rweyemamu,
Mulamu Nghambi, Madaraka Suleiman na Amina Poyo.
Kamati ya Mashindano itaongozwa na mwenyekiti Mohammed
Nassor, huku Makamu mwenyekiti akiwa ni Iddi Kajuna na Wajumbe wengine ni Jerry
Yambi, Hussein Simba na Mohammed Omar.
Kwa mamlaka aliyonayo kikatiba, Aveva amewateua Mohammed Nassor, Musleh Al Ruwaih na Salim
Abdallah kuwa wajumbe wa Kamati ya
Utendaji.
Katika hatua nyingine kikao kilichokaa jana kwa
mara ya kwanza tangu Aveva aingie Madarakani kiliamua
kuwasimamisha uanachama, wanachama 69 waliokwenda Mahakamani kuweka
zuizi la uchaguzi kufanyika.
Aveva alieza kuwa maamuzi hayo yamefanyika ili
kuilinda katiba ya Simba inayokataza masuala ya klabu kupelekwa katika mahakama
za kawaida.
Suala kama hilo liliwahi kufanywa na Michael
Richard Wambura mwaka 2010 na lilimgharimu katika uchaguzi wa mwaka huu.
Hata hivyo katika uchaguzi wa juni 29, Wambura
alizuiliwa kupiga kura kwa madai ya uanachama wake kuwa na utata.
Lakini suala la Wambura na wanachama wengine
kusimamishwa litaamuliwa katika mkutano mkuu wa wanachama unaotarajia kufanyika
agosti 3 mwaka huuu. Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment