
BAADA ya taarifa kuenea mchana wa leo kuwa
aliyekuwa kiungo mzoefu wa Yanga, Athumani `Idd Chuji` amesajiliwa na Azam
kutokana na kuonekana katika mazoezi ya klabu hiyo kwenye uwanja wa Azam
Complex, uongozi wa mabingwa hao umekanusha taarifa hizo.
Chuji aliyetemwa na Yanga alionekana katika jezi
ya Azam fc, lakini msemaji wa klabu
hiyo, Jafar Idd Maganga amesema klabu
hiyo haijaingia mkataba wowote na kiungo huyo.
Jafar aliongeza kuwa Chuji aliomba kufanya mazoezi
na Azam na kwasababu klabu hiyo inapenda michezo haikuona sababu ya kumnyima
nafasi hiyo.
“Chuji aliomba kufanya mazoezi, uongozi ukaona si
jambo la busara kumkatalia”. Alisema Jafar.
“Hata katika mazoezi ya leo jezi aliyovaa haikuwa
na namba yoyote, kwahiyo hatuna mkataba wowote”.
Jafar alisisitiza kuwa jioni ya leo ameongea na
katibu mkuu wa klabu hiyo, Nassor Idrissa `Father` na alielezwa kuwa hakuna
mkataba wowote ambao Azam fc imeingia na Chuji zaidi ya kuomba kufanya mazoezi.
‘Kuvaa jezi ya Azam sio kwamba ndio tumemsajili,
sisi tunaenda kisasa. Tunapofanya mazoezi, timu moja inavaa jezi na timu nyingine
inavaa jezi. Kama mchezaji yupo mazoezini lazima avae jezi, lakini hatuna
mkataba na mchezaji huyo”.
Hata hivyo, Jafar alisema suala la Chuji kusajiliwa itategemeana na mwalimu atamuonaje katika mazoezi na kama ataonekana ana kiwango kizuri, kazi ya uongozi ni kutekeleza mahitaji ya mwalimu.
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment