Friday, 8 August 2014

WHO yasema kwa sasa 'Ebola ni janga la kimataifa'


Idadi ya watu waliofariki kutokana na Ebola Afrika Magharibi inasemekana kufika 900
Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuenea kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa afrika kama janga la kimataifa linalohitaji kushughulikiwa kwa dharura.
WHO imesema kuwa mataifa yalio na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo hayana uwezo wa kudhibiti kiwango cha virusi hivyo na hivyo basi yanahitaji usaidizi wa kimataifa.
Tangazo hilo linajiri baada ya mazungumzo ya dharura mjini Genevakuhusu uwezekano wa kutuma wataalam wa ugonjwa wa maambukizi ili kuudhibiti ugonjwa huo ambao ni hatari zaidi.
Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu mia tisa magharibi mwa afrika .
Mataifa yalioathiriwa vibaya ni Guinea,Liberia na Sierra Leone,lakini pia visa vimeripotiwa nchini Nigeria.

0 comments: