Wachezaji saba wa Ujerumani, wanaugua mafua , saa
24 kabla ya mechi yao ya robo fainali dhidi ya Ufaransa.
Kocha Joachim Low anasema kuwa wengi wanaumwa na
koo ingawa hakutaja majina ya wachezaji wagonjwa.
"Ni mapema sana kufanya uamuzi wowote kuhusu
orodha ya wachezaji watakaoingia uwanjani, '' alisema Low
Mats Hummels na Christoph Kramer waliugua mapema
wiki hii huku Mat akikosa mechi ya muondoano dhidi ya Algeria Jumatatu.
Low anaamini kuwa mazingira ya Brazil na safari za
hapa na pale nchini humo pamoja na mvua kubwa ndio sababu ya wachezaji wake
kuugua.
Lakini aliongeza kuwa , hali sio mbaya sana ,
sitaki watu wadhani kuwa tunakabiliwa na wakati mgumu, hapana, '' alinukuliwa
akisema Low
Chanzo:BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment