Hatua ya robo fainali ya kombe la
dunia inaendelea leo. Saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika mashariki, Ufaransa
watachuana na Ujerumani.
Saa 5:00 usiku, wenyeji Brazil
watakuwa kibaruani dhidi ya Colombia.
Kfikia sasa hizi ndio takwimu muhimu
za kombe la dunia mwaka 2014, nchini Brazil.
Kufikia sasa mpaka michezo 56 kati ya
64 imekwishachezwa,
Takwimu muhimu mpaka sasa,
Mfungaji bora anayeongoza akiwa ni
James Rodrguez wa Colombia mwenye mabao matano, huku Neymar, Lionel Messi na
Thomas Muller wa Ujerumani wakifuatia wakiwa na mabao manne kila mmoja.
Jumla ya mabao 154 yamefungwa mpaka
sasa, ikiwa ni wastani wa mabao matatu kwa kila mechi.
Mechi iliyoshuhudia mabao mengi zaidi
yakifungwa ikiwa ni kati ya Uswiss na Ufaransa, ambapo jumla ya mabao saba
yaliingia wavuni.
Uholanzi ndo timu iliyofunga mabao
mengi zaidi mpaka kwenye michuano hii ikiwa na jumla ya mabao 12, mabao 11
yakifungwa kwa kupeana pasi huku bao moja likiwa ni kwa mpira uliokufa.
Ubelgji ndo timu iliyofanya
mashambulio mengi sana langoni mwa timu pinzani, ikiwa imefanya mashambulizi 81
kwa timu zote ilizokutana nazo, huku Algeria ikiwa ndo timu iliyokaba sana na
kuzuia mashambulizi mengi.
Ujerumani, Ni mabingwa wa kupiga pasi
nyingi zaidi ambapo hadi sasa wamekishapiga pasi 2560. Ila Javier Macherano wa
Argentina ndiye kinara wa kupiga pasi nyingi zaidi kwa wachezaji, akipiga jumla
ya pasi 364.
Michael Bradely wa Marekani, ni Usain
Bolt wa michuano hii akiwa ndiye mchezaji aliyekimbia sana uwanjani, akikimbia
kwa jumla ya mile elfu 54, 709 sawa na kilometa elfu 88 na 45.
Kwa upande wa Makipa, Kelya Navas
mlinda mlango wa Costa Rica ndiye kipa aliyeokoa michomo mingi zaidi kwenye
michuano ya mwaka huu, ambapo amekwisha okoa michomo 14 iliyoelekea langoni
huku akiruhusu kufungwa mabao mawili pekee.
Lakini mlinda mlango wa Nigeria,
Austine Edje naye amejiandikia rekodi mpya ya kuwa mchezaji aliyeitwa kwenye
kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria kwenye fainali tatu za michuano ya kombe la
dunia lakini hajacheza hata mechi moja.
Rafael Marquez wa Mexico amekuwa
nahodha aliyecheza fainali nne za michuano ya kombe la dunia, akianza toka
mwaka 2002 nchini Japan hadi sasa Brazil ambapo timu yake ilitolewa na Uholanzi
katika hatua ya kumi na sita bora.
Akiwa na umri wa miaka 43 Faryd
Mondragon, mlinda mlango wa Colombia amevunja rekodi ya mkongwe wa Cameroon,
Rogger Millar kwa kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kucheza mechi za kombe
la dunia.
Naye Kinda wa Marekani anayekipiga
kwenye klabu ya Bayern Munich, Julien Green amekuwa mchezaji wa saba kijana
kufunga bao akiwa na umri mdogo kwenye michuano ya kombe la dunia, akiwa kwenye
kundi moja na Lionel Messi wa Ajentina na Divock Origi wa Ubelgji.
Na
Kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya
mwaka huu, vinara wa makundi wamefuzu kwa hatua ya robo fainali, wakishindwa
kufungwa na timu zilizoshika nafasi ya pili kwenye makundi.
0 comments:
Post a Comment