Monday, 13 January 2014

LEO MPYA: GIROUD FITI KWA VILLA, ALLEGRI ‘APIGWA SHOKA’ AC MILAN, NASRI NJE WIKI 8!

SOMA ZAIDI:
GIROUD FITI KUIVAA VILLA LEO
NASRIHuku wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa Mastraika baada kuumia Theo Walcott na Nicklas Bendtner, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amepata faraja kubwa baada Mshambuliaji wake Olivier Giroud kupasishwa kuwa fiti kwa Mechi ya Leo ya Ligi Kuu England huko Villa Park dhidi ya Aston Villa ambayo ushindi kwa Arsenal utawarudisha tena kileleni walikokaa Man City.
Giroud alikuwa nje tangu afunge Bao la Ushindi Arsenal ilipoichapa Newcastle United Bao 1-0 hapo Desemba 29 baada kupata Jeraha na kuchanika Enka yake.
Nicklas Bendtner aliumia hapo Januari 1 wakati akifunga kwenye Mechi na Cardiff City waliposhinda 2-0 na anatarajiwa kuwa nje kwa Wiki kadhaa wakati Theo Walcott aliumia vibaya Goti kwenye Mechi iliyofuatia ya FA CUP waliyoifunga Tottenham 2-0 na atakuwa nje kwa Miezi 6.
Lakini hivi karibuni, Straika wa Germay Lukas Podolski alirejea Uwanjani baada kuwa nje kwa Miezi kadhaa akijiuguza Mguu wake.
AC MILAN: MASSIMILIANO ALLEGRI AFUKUZWA!
Siku moja baada kuchapwa 4-3 na ‘Timu mbovu’ Sassuolo, Vigogo wa Italy, AC Milan, wameamua kumtimua Kocha wao Massimiliano Allegri.
AC Milan, ambao wameshawahi kuwa Mabingwa wa Italy mara 18, wapo Nafasi ya 11 kwenye Ligi ya Serie A na wapo Pointi 30 nyuma ya Vinara Juventus.
Allegri, mwenye Miaka 46, ambae alitarajiwa kuondoka mwishoni mwa Msimu baada Mkataba wake kumalizika, ametimuliwa pamoja na Wasaidizi wake wote.
Kocha Msaidizi Klabuni hapo, Mauro Tassotti, ambae ni Mchezaji wa zamani wa AC Milan, amepewa kazi ya kukaimu Nafasi iliyoachwa wazi.
Tassotti, mwennye Miaka 53, alikaa kwa Miaka 17 kama Mchezaji hapo Sa Siro na amekuwa Kocha hapo tangu astaafu Soka Mwaka 1997.
Klabu nyingine ya Serie A ambayo imemtimua Meneja wake hii leo ni Livorno ambao wako Nafasi ya 19 na wamemfukuza kazi Davide Nicola.
SAMIR NASRI: NJE WIKI 8!
Kiungo wa Manchester City Samir Nasri leo amethibitishwa kuwa atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 8 baada kuumia Goti hapo Jana huko Saint James Park walipoifunga Newcastle Bao 2-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Nasri aliumizwa alipopigwa Buti Gotini na Mapou Yanga-Mbiwa ambae alipewa Kadi ya Njano kwa kitendo hicho.
Akithibitisha habari hizi kwenye Mtandao wake wa Twitter, Nasri aliposti: “Nadhani ni habari njema kuwa nje Wiki 8. Asante wote kwa kunipa sapoti na kunitakia mema!”
Mara baada ya Mechi ya Jana, Meneja wa City, Manuel Pellegrini, alionyesha wasiwasi wake aliposema Nasri ameumia vibaya lakini hii leo, baada uchunguzi wa kina, imethibitika maumivu yake si mabaya sana.

Related Posts:

0 comments: