>>SIMBA 0 KCC 1!!
>>
Shujaa wa KCC ni Herman Wasswa aliefunga
Bao pekee la Fainali hii katika Dakika ya 20 baada kupokea Krosi kutoka
Habib Kavuma na kumtambuka Beki Mkenya Donald Musoti na kumchambua Kipa
Ivo Mapunda.
Hii ni mara ya pili kwa KCC na Simba
kukutana kwenye michuano hiyo baada kutoka 0-0 katika hatua za Makundi
na hii ni mara ya kwanza kwa Simba, inayofundishwa na Kocha toka Serbia
Zdravko Logarusic, ‘kutobolewa’ kwa Bao katika Mashindano hayo.
Mbali ya kunyakua Kombe, KCC pia wamezoa zawadi ya Dola 10,000 kama Mabingwa.
Kwenye Ufungaji Bora, Kiungo wa URA,
Owen Kasule, alitwaa Tuzo ya Ufungaji Bora akiwa na Bao 4 na Herman
Wasswa, wa KCC, na Amri Kiemba, wa Simba, wanafuatia wakiwa na Bao 3.
MATOKEO:
ROBO FAINALI
Jumatano Januari 8
Gombani Stadium, Pemba
KMKM 0 URA 1
Azam FC 2 Clove Stars 0
Amaan Stadium
Tusker 0 KCC 0 [KCC imesonga kwa Penati 4-3]
Simba 2 Chuoni 0
NUSU FAINALI
Ijumaa Januari 10
Azam FC 2 KCC 3
URA 0 Simba 2
FAINALI
Ijumaa Januari 13
Amaan Stadium
Simba 0 KCC 1
0 comments:
Post a Comment