Picha juu na chini ni magari ya
kuzolea taka ngumu ya kampuni mbalimbali yakiwa kwenye foleni ya kuingia
Dampo la Pugu Kinyamwezi ambalo miundo mbinu yake ni mibovu na
kupelekea zoezi hilo kuchukua zaidi ya siku 4 mpaka kufanikisha kufikia
eneo maalum la kumwagia taka ngumu.
.Ni kutokana na kukwama kwa magari ya taka kwenye Dampo la Pugu
.Siku ya tatu sasa magari ya taka yamekwama
Na.Mwandishi wetu, MOblog
MIUNDOMBINU mibovu katika Dampo kuu
la jiji la Dar es Salaam Pugu Kinyamwezi imesababisha magari makubwa ya
kuzoa na kumwaga taka kukwama kwa muda wa siku tatu na kupunguza ufanisi
wa kuzoa taka katika mkoa wa Dar es Salaam, MOblog inaripoti.
Mtoa taarifa wetu ambaye hakutaka
kutajwa kwenye blogu hii, amesema kwamba uongozi wa Dampo Pugu umeshidwa
kuweka utaratibu mzuri na kukarabati miundombinu ya dampo kwa muda
mrefu na kusababisha msongamano mkubwa wakati wa kwenda kumwaga taka
katika sehemu hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa
MOblog jana asubuhi, mtoa taarifa (Jina linahifadhiwa) amesema kwa muda
wa wiki mbili sasa umwagaji wa taka katika dampo hilo siyo mzuri kabisa
na inaweza kufika miezi kadhaa tangu dampo hilo lianze kuelemewa na
uchafu kutoka kila kona ya jiji la Dar es Salaam.
“hali ni mbaya katika dampo la pugu
kwa miezi kadhaa sasa na uongozi wa dampo wameshidwa kufanya kazi kwa
tija na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa dampo katika jiji
la Dar es Salaam,’ amesema mtoa taarifa
Amesema magari makubwa aina ya
(Bulldozers) hayawafanyi kazi kabisa na kusababisha kukwama kwa kazi ya
kumwaga taka katika dampo la Pugu Kinyamwezi na msongamano mkubwa wa
magari.
Mtoa taarifa anasema kuwa kutokana na
matatizo hayo katika dampo la Pugu imesababisha baadhi ya taka kuoza
kabisa na kuleta harufu kali kwa wakazi wa karibu wa dampo hilo na
tishio la magonjwa ya mlipuko ni kubwa.
“kutokana na tatizo hili katika dampo
la hapa Pugu hali za kiafya kwa wakazi wa karibu wa eneo ni ya hatari
na magonjwa ya mlipuko yako mbioni kutokea,” aliongeza.
Pichani juu na chini hii ndio
hali halisi ya muonekana wa eneo la Dampo la Pugu Kinyamwezi. Kwa hali
hii kweli jamani hata hayo magari ya kuzoa taka yaliyopewa zabuni ya
kukusanya taka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam yatadumu
kweli....???
Hivi karibuni waandishi wa habari
ikiwemo blog hii walitembelea eneo la dampo na kufanya mahojiano na
badhi ya madereva, Devera wa gari la Kampuni ya usafi ya Green Waste
Pro ltd Bw. Ramadhani Sufi alisema adha wanayoipata ni pamoja na kulala
siku mbili na gari lenye mizigo ya taka katika mazingira ambayo
hawawezi kula kitu kwa hofu ya kupata magonjwa ya mlipuko kama
Kipindupindu.
‘tunawaomba viongozi wa jiji
kurekebisha hali hii ili waweze kutuepusha na magonjwa hatarishi
kutokana na uchafu unaorundikana mahali pamoja kuanzia kwenye dampo hadi
kwenye magari,” alisema.
Kwa upande wake Dereva Rajab Kavuzi
wa kampuni ya Tirima Enterprises, amefafanua kuwa hali hiyo
inasababisha kuwachafulia jina la kampuni yao na kuonekana kama
hawafanyi kazi kumbe tatizo lipo kwenye utaratibu mzima wa Manispaa na
suala la miundo mbinu.
Kwa upande dereva mwingine Bw.
Likongo wa Eco Protection alisema kero ya kwenye dampo la taka lililopo
maeneo ya Pugu Kinyamwezi ni za muda mrefu ambapo taka zimerundikana
hadi barabarani na njia hazipitiki hata Magreda ya kuzoa hayana
pakupita.
Gari la kampuni ya Tirima Enterprises likipita kwa shida kuelekea eneo maalum la kumwagia taka ngumu.
MOblog ilifanya jitihada za kumtafuta
Mkuu wa Afya Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam Bw.
Membe Protus Membe ambaye aliahidi kupambana na tatizo la mrundikano wa
magari ya taka yaliyokwama katika eneo la Dampo kutokana na ubovu wa
miundo mbinu ya barabara unaopelekea kukwamisha zoezi la ukusanyaji taka
katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar na kusababisha mrundikano wa
taka nyingi kwa muda wa siku tatu.
Lakini mpaka sasa hali iko hivyo
hivyo na imechukua takribani miezi sita tangu atoe ahadi hiyo ya kutatua
kero na ubovu wa miundombinu kuelekea dampo la Pugu Kinyamwezi.
0 comments:
Post a Comment