Afisa Wanyamapori wa Wilaya ya Singida, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya wanyamapori.
Afisa huyo, Augustino Lori alikamatwa jioni ya siku ya Jumatatu baada ya kukutwa amehifadhi ndege 12 aina ya flamingo, na silaha mbili aina ya bunduki, nyumbani kwake, kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Geoffrey Kamwela amesema afisa huyo anayepaswa kulinda maliasili, amekuwa

akituhumiwa
mara kwa mara na wananchi kuwa anamiliki silala bila kibali na
kujihusisha na vitendo vya uwindaji pamoja na usafirishaji haramu wa
wanyama pori.
Siku ya tukio, wananchi walitoa taarifa ambapo askari walifika kwa mtuhumiwa na kukuta ndege kadhaa kwenye chumba cha uani katika nyumba ya mtuhumiwa na baada ya kupekuliwa zaidi, ndipo zilipopatikana silaha hizo mbili moja ikiwa na risasi tatu, ambapo mbili zilikuwa za shortgun na moja ya rifle, zote zikiwa zimefichwa chini ya gorodo kwenye kitanda chumbani kwa mtuhumiwa.
Kamanda Kamwela amesema mtu mwingine aitwaye Hamza Ali, naye alikamatwa na polisi akiwa katika harakati za kuwatega ndege huko katika ziwa Singidani.

0 comments:
Post a Comment