Tuesday, 7 January 2014

HII NDIO SIRI YA ZITTO KUSHINDA KESI JANA DHIDI YA KAMATI KUU YA CHADEMA

Jaji John Utamwa wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ameridhia ombi la pingamizi lililotolewa  na Zitto Kabwe dhidi ya kujadiliwa kwa uanachama wake au kuchukuliwa hatua zozote na Kamati Kuu ya CHADEMA. Jaji Utamwa amekitaka chombo hicho ama kingine kutii amri hiyo mpaka hapo rufaa ya Zitto itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi na  Baraza Kuu la chama hicho kama ilivyoombwa.

Habari kamili

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,  imeamuru Kamati Kuu ya CHADEMA kutojadili uanachama wa aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.

Amri hiyo imo katika uamuzi wa Jaji John Utamwa, ambaye amekubali hoja za upande wa Zitto, ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Alisema kwamba hoja zake zimekidhi matakwa ya kisheria ya kutolewa kwa zuio la muda la kutojadiliwa kwa uanachama wake.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Utamwa alisema Kamati Kuu ya chama hicho au chombo chochote cha CHADEMA, hakitaruhusiwa kujadili suala la uanachama wa Zitto hadi kesi yake ya msingi aliyoifungua mahakamani itakaposikilizwa.

Zitto amefungua kesi dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chama hicho na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa, akiiomba Mahakama itoe zuio hilo, hadi atakapokata rufaa ya kupinga uamuzi uliomvua uongozi wa chama.

Aidha anaiomba Mahakama imwamuru Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Slaa ampe nakala zinazotoa sababu za uamuzi wa kumvua uongozi katika kikao kilichofanyika Novemba 22 mwaka jana, ili akate rufaa katika Baraza Kuu la Chama.

Katika uamuzi wake Jaji Utamwa alisema kwa mujibu wa Sheria ili Mahakama itoe zuio, ni lazima katika suala la msingi kuwe na mtu ambaye atapata madhara ambayo hayatarekebishika.

Alisema katika ombi la Zitto, amekidhi matakwa ya kisheria, kwa kuwa zuio hilo lisipotolewa na akavuliwa uanachama, atapoteza nafasi ya ubunge na kushindwa kuwatumikia wananchi waliomchagua na pia atapoteza nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge wa Kamati ya Kudumu ya  Hesabu za Serikali.

Jaji Utamwa alisema endapo Zitto atavuliwa uanachama kabla hajapewa haki ya kusikilizwa, atapata madhara makubwa ambayo hayarekebishiki hata kama uchaguzi utafanyika tena.
 
Siri ni kua ombi la Zitto, limekidhi matakwa ya kisheria, kwa kuwa zuio hilo lisipotolewa na akavuliwa uanachama, atapoteza nafasi ya ubunge na kushindwa kuwatumikia wananchi waliomchagua na pia atapoteza nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge wa Kamati ya Kudumu ya  Hesabu za Serikali.

0 comments: