HUKU
Cristiano Ronaldo akiibuka kuwa ndio anaetegemewa kutwaa Tuzo ya
Mchezaji Bora Duniani, Ballon d'Or, Staa wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic,
ameibuka na kudai yeye ni bora na hivyo hahitaji Ballon d'Or.
Ibrahimovic, ambae Msimu uliopita
aliisaidia Klabu yake PSG kutwaa Ubingwa wa Ligue 1 huko France,
aliwaambia Wanahabari hapo Jana: “Sihitaji Ballon d'Or ili kujua mimi ni
bora. Hiyo ni muhimu kwa Wachezaji wengine.”
Jumatano, Ibrahimovic alifunga Bao lake
la 39 kwenye UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, wakati PSG inaifunga Olympiakos
2-1 Uwanjani Parc des Princes na kushinda Nafasi ya Kwanza ya Kundi lao
na pia kufuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 wakiwa na Mechi moja
mkononi.
Haijapata kutokea Mchezaji kutoka Sweden akatwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani lakini hilo halimnyimi Ibrahimovic usingizi.
Amefafanua: “Si kitu ambacho ninakifikiria na si kitu muhimu kwangu!”
Mshindi wa Ballon d'Or atatangazwa hapo Januari 13.
Hivi sasa lengo la Ibrahimovic ni
kuisaidia PSG kutetea tena Ubingwa wao ambapo Jumapili watakuwa Nyumbani
kucheza na Olympique Lyon huku Klabu yake ikiwa ndio inaongoza Ligue 1
ikiwa na Pointi 34 kwa Mechi 14.
0 comments:
Post a Comment