SUPASTAA
kutoka Argentina anaechezea Klabu ya FC Barcelona, Lionel Messi, leo
Jumatano atatunukiwa kiatu/Buti ya Dhahabu baada kuwa Mfungaji Bora kwenye
Ligi za Juu Barani Ulaya kwa Msimu uliopita.
Hii itajuwa mara ya 3 kwa Messi kushinda Tuzo hiyo kwani alishaitwaa kwenye Misimu ya 2009-10 na 2011-12.
Sherehe za kumzawadia Tuzo hiyo zitafanya huko Antigua Fábrica de Damm Jijini Barcelona hivi leo.
Tuzo hii ya Buti ya Dhahabu hutolewa na
European Sports Media (ESM), ambayo ni Jumuia ya Wachapaji wa Majarida
makubwa ya Michezo hukoUlaya
yakiwemo A Bola, Fanatik, Elf Voetbal, Kicker, Sport Express, Sport
Voetbal, Tipsbladet, Titan Media, Telesport, Frankfurter Allgemeine,
World Soccer, Kick Off, sports.163.com, Sportal Korea na MARCA.
SUAREZ KUPELEKEWA NDEGE MAALUM ILI AWAHI DABI YA MERSEYSIDE!
STRAIKA wa Liverpool Luis Suarez
atapelekewa Ndege binafsi ya Mmiliki wa Liverpool, Mmarekani, John W
Henry, ili awahi kurudi Jijini Liverpool kuiwahi Mechi ya Ligi Kuu
England dhidi ya Everton kutoka kwao Montevigeo, Uruguay ambako Nchi
yake itapambana na Jordan Jumatano katika Mechi ya Marudiano ya Mchujo
wa Kimataifa ili kwenda Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Amman, Jordan, Uruguay ilishinda Bao 5-0.
Mechi hiyo ya Everton na Liverpool,
mtanange mkali wa Dabi ya Merseyside, itachezwa Jumamosi Mchana na kama
hatapelekewa Ndege maalum, Suarez atarejea Jijini Liverpool Ijumaa na
hivyo kuwepo mashaka kama ataicheza Dabi hiyo.
0 comments:
Post a Comment