Dar es Salaam. Mwenyekiti wa
Chadema Mkoa wa Lindi, Ally Chitanda, ametangaza kujiondoa katika nafasi
hiyo akieleza kuchoshwa na uamuzi wa kikanda na kikabila unaoendelea
ndani ya chama hicho.
Mbali na Uenyekiti, Chitanda pia
alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa na Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu-
Sekretarieti nafasi ambayo pia alitangaza kujiuzulu jana, lakini
akaahidi kuendelea kuwa mwanchama mwaminifu wa Chadema.
Hata hivyo katika maelezo yake ya sababu za
kujiuzulu alisema: “Sioni sababu ya kuendelea kuwa mwana Chadema, sioni
sababu ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi.”
“Sioni sababu ya kuwa kiongozi kwa kuwa kipaumbele
cha Chadema ni kukijenga chama Kaskazini, basi sisi wa Lindi
tunawatakia kila la heri….”
Alisema amefikia hatua hiyo baada ya uamuzi wa
Kamati Kuu ya Chama hicho, kuwavua nyadhifa Zitto na mwenzake Dk Kitila
Mkumbo wiki iliyopita.
Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa kuhusu uamuzi huo
wa Chitanda alisema kuwa hawezi kumzunguzia kwa kuwa ni mtu mdogo katika
chama akitaka atafutwe msemaji wa Chadema Tumaini Makene aliyesema:
“Mwambieni Chitanda atoe barua ya uteuzi wake.”
Na Ibrahim Yamola, Mwananchi
Posted Jumapili,Decemba1 2013
Posted Jumapili,Decemba1 2013
0 comments:
Post a Comment