Tuesday, 19 November 2013

50 wafukiwa baada ya jengo kuporomoka South Afrika

 
Wengi wa waliofukiwa wanaaminika kuwa wajenzi
Takriban watu 50 wamekwama kwenye vifusi baada ya paa ya jumba la maduka lililokuwa linajengwa kuporomoka nchini Afrika Kusini.
Inaarifiwa watu 29 wameweza kuokolewa na mwingine mmoja kuthibitishwa kufariki.
Madaktari kutoka kampuni ya kibinafsi ya Netcare 911 walifika kutoa huduma ya kwanza katika eneo hilo la Tongaat Kaskazini mwa mji wa Durban.
“Shughuli hii itachukua mda mrefu. Itatuchukua muda kuwafikia wale waliokwama,” alisema msemaji wa kampuni hiyo.
Hata hivyo ni mapema mno kujua sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo.
Inaarifiwa watu wengine 26 wamepelekwa hospitalini wakiwa na majereha mabaya.

0 comments: