Sunday, 17 November 2013

HIVI TEVISHENI YA TAIFA NI IPI? TBC ONE AU ITV MTAZAMO TU :SOMA HAPA KUJUA''''''''''

Napata sana shida kuelewa na kujua umuhimu wa TBC kama ni kweli shirika hili ni kwa ajili ya Taifa kweli au ni shirika linalofanya kazi kwa matuko yanayohusu kikundi kidogo cha watu wazito hususani wenye power.

Nimeandika hivyo kwa sababu ya mambo yanavyokwenda inasikitisha sana kujua kama kunahitajika usawa wa kupata habari na kutoa habari kwa wananchi kuhusu mustakabali wa matukio yanayohusu Taifa kwa ujumla.

Kama Taifa wananchi tunakatwa kodi ili shirika liweze kutoa habari na wananchi tuweze kujuzwa mambo yanavyokwenda. Nimeandika haya kwa sababu naiona nafasi ya TBC kama chombo cha Taifa cha kutoa HABARI, ELIMU NA BURUDANI 
kinakosa sifa hizo na kwenda kwenye chombo cha mtu binafsi.

Inasikitisha,inaumiza na kuhuzunisha sana kuona matukio muhimu kabisa yanayohusu au kuligusa Taifa hayapewi kipaumbele. ITV kama chombo cha mtu binafsi kanachukua nafasi ya kuwa chombo cha KITAIFA kwa uzembe wa watu waliopewa nafasi ya kuongoza.

Tunasistizwa kuwa wazalendo lakini wao wenyewe wanashindwa kutuonesha kwa vitendo linapokuja suala la uzalendo.

Taifa loote kwa maana ya Viongozi wa kitaifa kasoro RAIS J KIKWETE labda na mzee MWINYI ndio hawakuwepo pale Karimjee ila Rais Mstaafu Mkapa, Makamu wa Rais Bilal, Mh Pinda na viongozi wa vyama karibu woote wa vyama vya siasa walikuwepo katika sherehe ya kuuaga mwili wa Dk MVUNGI kwa nini TBC chombo cha umma wasioneshe moja kwa moja?

Inauma saana kwa mtu ambae amelipigania Taifa kutopewa kipaumbele na Chombo cha Taifa.
--- Nyanya mbichi via JF


TBC1 kama TV ya Taifa ilipaswa kuonesha tukio la kuuaga Mwili wa Mzalendo Dr. Mvungu lakini badala yake walikuwa wanaonesha tamthilia ya kichina muda huo huo! Hii tafsiri yake kuwa wao hawajaguswa na tukio hili?
--- The Quest via JF


TBC 1 walikuwa wanaonesha muziki wa taarabu wakati tayari taifa lina taaharuki ya meli kuzama na kuua halaiki ya watu huko Zanzibar sembuse Dr Mvungi?
---  MTAZAMO via JF


Soma Comments hizi

ER
16/11/2013 18:45
TBC ni television ya serikali na propaganda ya chama tawala. Nafikiri ITV ikokaribu ya kuwa television ya taifa.
Nakumbuka zamani ilikuwa inaitwa television ya taifa nafikiri walibadili jina baada kuona maudhui ya chombo chao hayalingani na jina! Ninaweza kuwa nimekosea
Reply
 
16/11/2013 18:56
Cha kushangaza sana leo hata kuiona TBC1 hewani haikuonekana kipindi chote cha kuaga mwili wa Dr mvungi na iliporudi hewani tuu ilirudi na chereko na bango na baadaye tamthilia ya ajabu sana ya Kichina!!!!!! Naungana na wadau kuitambua ITV kama Tv ya taifa......ukisikia wakurugenzi waliofeli nadhani Mshana na bodi ya wakurugenzi tbc wakubali kushindwa
Reply
 
mwambungu
16/11/2013 21:35
hivi mpaka sasa mlikuwa hamjui kama tbc1 ni ya watu binafsi?mbona soku nyingi sana.!hivi hamuoni hata maudhui ya utangazaji wao ni uccm zaidi kuliko utaifa hamkumbuki ile ya tido mhando,alipo buni kipindi cha wagombea kujieleza akaonekana ni mchochezi. Kwa sasa ITV NDIYO TV YA TAIFA MAMBO YOTE YAHUSUYO MASLAHI YA TAIFA YAPO ITV VIPINDI VIZURI KAMA MALUMBANO YA HOJA NA KIPIMA JOTO, wakatae wakubali ITV NDIYO TV YA TAIFA ukweli unauma.
Reply
 
Israel
17/11/2013 06:15
Ukiona hayo yanatokea, mteule uwe macho. Kumbuka maneno haya, "Pasipo maono, watu huangamia". TBC hawana maono yo yote zaidi ya kuiba maono ya wengine.

TBC watavizia vipindi vinavyopendwa sana na wananchi kupitia Television zingine, kisha badala ya wao kubuni vya kwao, watatafuta mbinu ya kuviiba, kwa maana ya wasanii / au wadamini. Mfano: ORIGINAL COMMEDY vs ZE COMEDY na Bongo Star Search.......... Poleni sana mnaoangalia TBC inayojifia yenyewe. 

 
         Chanzo wavutiblog

0 comments: