Saturday, 23 November 2013

BUNDESLIGA: BAYERN MUCHERN YAICHAPA DORTMUND 3-0! NA KUTUPWA NAFASI YA 3

BAYERN_MUNICH_LOGOMario Gotze, alitoka Benchi, na kuja kuiumbua Klabu yake ya zamani Borussia Dortmund kwa kuifungia Bayern Munich Bao la kwanza na kufungua njia ya ushindi wa Bao 3-0 katika Mechi ya Bundesliga iliyochezwa Signal Iduna Park.
Gotze hakushangilia Bao hilo la Dakika ya 66 dhidi ya Dortmund iliyokuwa ikicheza na Difensi ya kuungaunga baada ya Wachezaji wao mahiri wa nyuma kuwa majeruhi.
Bao la Pili la Mabingwa wa Germany, Bayern Munich, lilifungwa katika Dakika ya 85 na Arjen Robben na Bao la Tatu kupachikwa Dakika ya 87 na Thomas Muller.

Ushindi huo umewafanya Bayern wazidi kukaa kileleni wakiwa na Pointi 35 kwa Mechi 13 na kufuatiwa na Bayer Leverkusen wenye Pointi 31 huku Dortmund ikikamata Nafasi ya 3 ikiwa na Pointi 28.
VIKOSI:
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Groskreutz, Sokratis, Friedrich, Durm, S Bender, Sahin, Blaszczykowski, Mkhitaryan, Reus, Lewandowski.
Bayern Munich: Neuer, Rafinha, Boateng, Dante, Alaba, Martinez, Robben, Kroos, Lahm, Muller, Mandzukic.

0 comments: