Sunday, 17 November 2013

HIVI NDIVYO CAMEROUN ILIVYO TINGA BRAZIL KATIKA KOMBE LA DUNIA 2014

  YAIBONDA TUNISIA 4-1,  

...NI REKODI, NI MARA YA 6 FANAILI ZA KOMBE LA DUNIA

CAMEROUN leo huko Yaounde wameibonda Tunisia Bao 4-1 na kuwa Nchi ya 3 toka Afrika,CAMEROUN-SONGkufuatia Jana Nigeria na Ivory Coast, kufuzu kwenda Brazil Mwakani kucheza Fainali za Kombe la Dunia.

MAGOLI:
Cameroon 4
-Pierre Webo Dakika ya 4
-Benjamin Moukandjo 30
-Jean Makoun 66 & 86

Tunisia 1
-Ahmed Akaichi 51

Hii ni mara ya 6 kwa Cameroun kucheza Fainali za Kombe la Dunia na mara nyingine zikiwa Miaka ya 1982, 1990, 1994, 1998, 2002 na 2010 ambayo ni Rekodi kwa Afrika.


AFRIKA
RATIBA/MATOKEO:
Marudiano:

Jumamosi Novemba 16
Nigeria 2 Ethiopia 0
 [Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili 4-1]
Senegal 1 Ivory Coast 1
 [Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili 2-4]

Jumapili Novemba 17
Cameroon 4 Tunisia 1
 [Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili 4-1]

[Saa za Bongo]
[Katika Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Jumanne Novemba 19
19:00 Egypt v Ghana [1-6]
21:15 Algeria v Burkina Faso [2-3]

Kmbuka bado timu mbili 2 kufuzu  kwenda brazil katika kombe la dunia

0 comments: