Tuesday, 19 November 2013

GHANA NAYO YAKATA KETI YA KWENDA BRAZIL BAADA KUFUNGA 2-1

>>YAFUNGWA 2-1 MJINI CAIRO, YAPITA JUMLA BAO 7-3!!
GHANA Usiku huu imekuwa Nchi ya 4 toka Afrika, baada ya Nigeria, Ivory Coast na Cameroun, kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwezi Juni Mwakani licha ya kufungwa Bao 2-1 Mjini Cairo na Egypt.
Ghana walishinda Mechi ya kwanza huko Kumasi Mwezi uliopita kwa Bao 6-1 na hivyo wamefuzu kwa Jumla ya Mabao 7-3.

AFRIKA
RATIBA/MATOKEO:
Marudiano
Jumanne Novemba 19

Egypt 2 Ghana 1 [Jumla ya Mabao Mechi mbili 3-7]
[Saa za Bongo]
[Katika Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]

21:15 Algeria v Burkina Faso [2-3]

EGYPT_v_GHANA-19NOVEgypt ndio walitangulia kupata Bao 2, Bao moja kila Kipindi, kwa Bao za Amr Zaky, baada frikiki ya Gwiji Mohamed Aboutrika, na Bao la pili kupitia Mohamed Nagy-Gedo.
Bao la Ghana lilifungwa na Kevin Prince Boateng alieingia Kipindi cha Pili.
Baadae leo Timu ya 5 na ya mwisho kwa Afrika kwenda Fainali za Kombe la Dunia itajulikana baada ya Mechi ya huko Mjini Algiers kati ya Algeria na Burkina Faso ambapo Burkina Faso wako mbele kwa Bao 3-2 waliposhinda Mechi ya kwanza.
VIKOSI:
EGYPT: Sherif Ekrami – Hazem Emam, Rami Rabiea, Mohamed Naguib, Mohamed Abdel-Shafy – Hossam Ghaly, Ahmed Fathi – Mahmoud Abdel-Moneim 'Kaharaba', Mohamed Abou-Treika, Mohamad Salah, Amr Zaki.
GHANA: Fatau Dauda - Harrison Afful, Daniel Opare, Jerry Akaminko, Rashid Sumaila - Michael Essien, Andre Ayew, Sulley Muntari, Kwadwo Asamoah - Abdul Majeed Waris, Asamoah Gyan.
Refa: Noumandiez DOUE (Ivory Coast)

TIMU AMBAZO ZIMEFUZU KWENDA BRAZIL
[Jumla 25 Bado 7]:
Afika [Nchi 4 Bado 1]: Nigeria, Ivory Coast, Cameroun, Ghana
Europe [Nchi 9 Bado 4]: Belgium, Bosnia-Herzegovina, England, Germany, Italy, Netherlands, Russia, Spain, Switzerland
South America [Nchi 5, Uruguay wapo kwenye Nchujo]: Argentina, Brazil (Wenyeji), Chile, Colombia, Ecuador
Asia [Nchi 4, Jordan wapo kwenye Mchujo]: Australia, Iran, Japan, South Korea
North & Central America/Caribbean [Nchi 3, Mexico wapo kwenye Mchujo]: Costa Rica, Honduras, USA
Oceania[New Zealand wapo kwenye Mchujo]

0 comments: