Saturday, 30 November 2013

KOMBE LA SHIRIKISHO: TP MAZEMBE YASHINDA 2-1LAKINI BINGWA CS SFAXIEN!!

MBWANA SAMATTA APIGA BAO LA PILI!!
KLABU ya Tunisia CS Sfaxien leo imetwaa Taji lao la 3 la Kombe la Shirikisho huko LubumbashiMBWANA_SAMATTA_IN_TPlicha ya kuchapwa Bao 2-1 na TP Mazembe.

MAGOLI:
TP Mazembe 2
-Cheibane Traore Dakika ya 10
-Mbwana Ally Samata 23
Club Sportif Sfaxien 1
-Fakhreddine Ben Youssef Dakika ya 88

CS Sfaxien wametwaa Kombe baada ya kushinda Mechi ya kwanza Bao 2-0 iliyochezwa Jumamosi iliyopita kwenye Mji wa Sfax Nchini Tunisia na hivyo kuvikwa Ubingwa kwa Jumla ya Mabao 3-2.
Sfaxien wameshatwaa Kombe hili Mwaka 2007 na 2008 na 2010 walikuwa Washindi wa Pili.
Kwa kutwaa Kombe hili, CS Sfaxien wamezawadiwa Dola 660,000 na Mwezi Februari watacheza na Al Ahly ya Egypt kuwania CAF Super Cup.

0 comments: