KWA KUZIKUTANISHA OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA OFISI ZA MAKATIBU TAWALA NA WAKURUGENZI WA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA MIKOA YA RUKWA, LINDI, MARA, RUVUMA NA SHINYANGA

........................................................
Mkoa
wa Rukwa ni miongoni mwa Mikoa iliyowezeshwa kuwa na Miundombinu ya
huduma ya "Video Conference" ambao unaratibiwa na Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia. Huduma hii muhimu itasaidia sana katika
kurahisisha mawasiliano Serikalini na hivyo kupunguza gharama na
kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na utoaji huduma kwa wananchi.
Katika majaribio
ya awali Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imetoa mada
mbalimbali kupitia mfumo huo kwa Makatibu Tawala pamoja na Wakurugenzi
wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mikoa ya Rukwa, Mara, Lindi, Ruvuma
na Shinyanga.
Miongoni mwa mada hizo
zilizowasilishwa zikifuatiwa na majadiliano ni Utekelezaji wa Mfumo wa
"OPRAS" katika Utumishi wa Umma, Mwenendo wa utekelezaji wa
masuala Anuai za jamii katika Utumishi wa Umma, Usimamizi na uzingatiaji
wa Maadili ya Utumishi wa Umma na Mafanikio na Changamoto za
utekelezaji wa Mfumo wa Taarifa za kiutumishi na Mishahara Serikalini.
Zoezi
hili la majaribio limefanikiwa japo kumekuwepo na changamoto mbalimbali
ikiwemo kukatika kwa mawasiliano yanayounganisha picha na sauti sababu
kubwa ikiwa ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kukosa huduma za Mkongo wa
Taifa unaoratibiwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayanisi na Teknolojia.
Changamoto nyingine ni
baadhi ya picha kuwa na muonekano hafifu, ambayo kwa mujibu wa Mchambuzi
wa Mifumo ya Komputa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Ndugu Emmanuel
Mwandiga inasababishwa pia na kasi ya huduma za mtandao kuwa chini
pamoja na masafa ya mawasiliano kuwa hafifu.
Changamoto hizo
zikifanyiwa kazi na Wizara husika ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
ni wazi kuwa mfumo huo utakua njia sahihi zaidi na kisasa inayokwenda na
wakati katika kurahisisha na kuboresha mawasiliano Serikali.




0 comments:
Post a Comment