Tuesday, 26 November 2013

SIIPENDI NA NALAANI WANAFUNZI NA UNIFAORM KWENYE VIDEO ZA MIZIKI

Suala la kuwaweka watoto na uniform zao za shule kwenye miziki isiyo na mafunzo yoyote ya kuwasaidia katika masomo yao na maisha ni sawa kweli?

Kukata kiuno mbele ya teenagers tena na watu wanaoonekana sura zao ni watoto na vijana tena wakiwa na mavazi rasmi ya shule, kunatoa funzo gani kwa jamii nzima?

Who should speak against it?

Hivi watoto hawa wakifanya hivi ama zaidi ya hapo huko mashuleni maana ni umri wa mihemko, nani atalaumiwa?

Ni Walimu watakaobebeshwa lawama hapa?

Lipi jukumu la Wazazi, Wanafunzi na jamii inayotizama haya?

Binafsi siafiki wala sioni hili kuwa haki na sawa kwa wanafunzi, hata ikiwa jamii inaona ni sawa. Huku ni kuharibu kizazi.

Wanaharakati wa haki za watoto (wanaopigania malezi bora) mnapaswa kuongoza harakati za kukemea suala hili.

Sababu za kuzingatia:
  1. Wanatumiwa wanafunzi wakiwa na uniforms zao: Hii itahalalisha tukio zima kuwa ni sawa.
  2. mri walioushiriki watoto hawa unahitaji consent ya wazazi/walezi wao.
  3. Kucheza muziki wenye kuamsha ashiki na fikira za kujaribu ngono mbele ya watoto ambao sio rika lao, mbele ya umma, haipo katika nchi yoyote iliyoendelea kwa hivyo hii siyo njia mbadala ya kulikuza na kuliendeleza Taifa bora.

Mdau,
Dk B. S.

0 comments: