Saturday, 30 November 2013

ALIYE BAKWA tFUTIWA MAASADA MOSHI

 
Moshi. Uongozi wa Kijiji cha Kiria, Kata ya Mamba Kusini wilayani Moshi, Kilimanjaro umeiomba Serikali na taasisi zinazojihusisha na ukatili wa kijinsia kumsaidia mtoto mwenye umri wa miaka 13 aliyebakwa na kulawitiwa na baba yake mzazi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Doroth Mtui alisema mtoto huyo kwa sasa amehifadhiwa kwenye nyumba ya msamaria mwema na anahitaji matunzo na kupelekwa shule, jambo ambalo serikali ya kijiji imeshindwa.
Mtui alisema mtoto aliyekuwa darasa la kwanza kabla ya kuachishwa shule, anahitaji kuishi sehemu tofauti na mazingira ya nyumbani ili kumnusuru na tatizo la kisaikolojia.
Mtui alisema mtoto huyo alipaswa kurudishwa hospitalini wiki mbili toka alipofanyiwa uchunguzi 0ktoba 9 mwaka huu, lakini mpaka sasa hajarudishwa kwa vile hakuna mwenye uwezo wa kumsaidia.
“Uchunguzi unaonyesha kuwa ameharibika vibaya sehemu za siri na ameota nyama kwa ndani. Alipewa dawa na anatakiwa kurudi tena kwa ajili ya uchunguzi,” alisema Mtui
.Na Rehema Matowo, Mwananchi
Posted  Jumapili,Decemba1  2013  

0 comments: