Thursday, 14 November 2013

KOMBE LA DUNIA-MCHUJO: MEXICO, URUGUAY ZAPIGA 5 KILA MMOJA!


NCHI za Mexico na Uruguay Jana zilipiga hatua kubwa kutinga Fainali za Kombe la Dunia za huko Brazil Mwaka 2014 baada kushinda Mechi zao za kwanza za Mchujo za Kimataifa.BRAZIL_2014_BEST
Mexico, wakicheza kwao Mexico City, waliitwanga New Zealand Bao 5-1 na Uruguay, waliokuwa Ugenini huko Jordan, waliwapiga Jordan Bao 5-0.
Nchi hizi zitarudiana Wiki ijayo na Washindi watapata Tiketi ya moja kwa moja kwenda Brazil Mwakani.
 
TIMU AMBAZO ZIMEFUZU KWENDA BRAZIL
[Jumla 21 Bado 11]:
Europe [Nchi 9 Bado 4]: 
 Belgium, Bosnia-Herzegovina, England, Germany, Italy, Netherlands, Russia, Spain, Switzerland
South America [Nchi 5, Uruguay wapo kwenye Nchujo]: Argentina, Brazil (Wenyeji), Chile, Colombia, Ecuador
Asia [Nchi 4, Jordan wapo kwenye Mchujo]: Australia, Iran, Japan, South Korea
North & Central America/Caribbean [Nchi 3, Mexico wapo kwenye Mchujo]: Costa Rica, Honduras, USA
-  
DROO YA KUPANGA MAKUNDI:
-KUFANYIKA TAREHE 6 DESEMBA 2013 Costa do Sauípe Resort, Mata de São João, Bahia, Brazil
-Kwenye Droo hiyo Timu 7, pamoja na BRAZIL, ambazo ziko juu kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani zitawekwa Chungu Na 1 na Timu nyingine 24 zilizobakia zitagawanywa nane nane na kuingizwa Vyungu vingine vitatu na kutenganishwa kutoka Mabara zinakotoka.
-FAINALI KUCHEZWA: 12 Juni 2014 hadi 13 Julai 2014


Kwenye ushindi wao, Bao za Mexico zilifungwa na Paul Aguilar, Raul Jimenez, Oribe Peralta Morones, Bao 2, na Rafael Marquez huku Bao la New Zealand Mfungaji akiwa Chris James.
Nao Uruguay walifunga Bao zao 5 kupitia Victorio Maximiliano Pereira Paez, Christian Ricardo Stuani, Nicolas Lodeiro Cristian Rodriguez, Edinson Cavani

VIKOSI:
JORDAN (4-4-2): Shatnawi, Nassar, Khattab, Al Murjan, Alsaify, Hasan, Ibrahim, Zahran, Bani, Aqel, Al Bashir
URUGUAY (4-4-2): Silva; Pereira, Lugano, Godin, Caceres; Arevalo, Stuani, Lodeiro, Rodriguez; Cavani, Suarez
KOMBE LA DUNIA
MECHI ZA MWISHO ZA MCHUJO:
**KWA AFRIKA, HIZI NI MECHI ZA MARUDIANO, Kwenye Mabano ni Matokeo Mechi ya Kwanza.
RATIBA/MATOKEO:
TAREHE SAA MJI TIMU TIMU KANDA
Nov-13 2330 Mexico City Mexico New Zealand CONCACAF/Oceania [5-1]
Nov-13 1800 Amman Jordan Uruguay Asia/South America [0-5]
Nov-15 2200 Piraeus Greece Romania ULAYA
Nov-15 2245 Lisbon Portugal Sweden ULAYA
Nov-15 2245 Kyiv Ukraine France ULAYA
Nov-15 2245 Reykjavik Iceland Croatia ULAYA
Nov-16 1800 Calabar Nigeria Ethiopia AFRIKA [2-1]
Nov-16 2200 Casablanca Senegal Ivory Coast AFRIKA [1-3]
Nov-17 1700 Yaounde Cameroon Tunisia AFRIKA [0-0]
Nov-19 1900 Cairo Egypt Ghana AFRIKA [1-6]
Nov-19 2115 Blida Algeria Burkina Faso AFRIKA [2-3]
Nov-19 2115 Zagreb Croatia Iceland ULAYA
Nov-19 2145 Solna Sweden Portugal ULAYA
Nov-19 2300 Saint-Denis France Ukraine ULAYA
Nov-19 2100 Bucharest Romania Greece ULAYA
Nov-20 0900 Wellington New Zealand Mexico CONCACAF/Oceania
Nov-21 0200 Montevideo Uruguay Jordan Asia/South America

0 comments: