Thursday, 21 November 2013

BAADA YA SIKU 14 MBUNGE MACHALI AMETOKO RUMANDE

MBUNGE wa Ukerewe, Salvatory Machemli (39), (CHADEMA) amepata dhamana baada ya kuwekwa rumande kwa siku 14 kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Mahakama ya Wilaya ya Ukerewe, ilifuta dhamana ya Machemli Novemba 6 mwaka huu na kuamuru awekwe rumande kwa 14 baada ya kushindwa kufika mahakamani zaidi ya mara tano bila taarifa wakati kesi yake ikitajwa.

Mbunge huyo anayekabiliwa na kesi ya uchochezi namba 19 ya mwaka huu, jana aliachiwa kwa dhamana baada ya
wadhamini watatu wenye hati za nyumba kama ilivyoamuliwa na Mahakama, kujitokeza kumdhamini.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Faustine Kishenyi alimtaka mbunge huyo kusalimisha hati zake za kusafiria na hatatakiwa kwenda nje ya wilaya bila kibali cha Mahakama.

Machemli baada ya kuachiwa kwa aliondoka mahakamani hapo akitembea kwa miguu huku umma mkubwa wa watu ukimfuata hadi Hoteli ya La Bima.

Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa Novemba 6 mwaka huu, imeahirishwa hadi Desemba 24 mwaka huu itakapotajwa tena ili mashahidi watatu kati ya watano waliosalia wa upande wa Jamhuri, waendelee kutoa ushaidi. --- 
 
via HabariLeo.

 

0 comments: