Tuesday, 26 November 2013

MWANAFUNZI AVUNJWA KIDOLE KWA KUADHIBIWA NA MWALIMU WAKE

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya Yetu blog — Mwanafunzi wa darasa la nne katika  shule ya msingi Airport Kata ya Iyela jijini Jaqueline Staniely, 9 ameumizwa mkono wake wa kushoto kwa kuvunjwa kidole.

Jacqueline akiongea kwa ridhaa ya mama yake amesema alipigwa kwa kutumia ubao na mwalimu wa shule hiyo Novemba 19 mwaka huu na mwalimu Kanyika kwa kosa la kuwa na nywele ndefu.

Mwanafunzi huyo amedai kuwa siku ya tukio alipigwa vibaya na kumsababishia maumivu makali ambapo siku hiyo mama yake alikuwa safarini Nairobi Kenya hivyo hakupata matibabu ambapo alilazimika kumwambia mwalimu jirani (Bibi) ambaye alimpeleka hospitali kutibiwa. 
 

0 comments: