Monday, 18 November 2013

MISRI YAOMBA MIUJIZA ILI WAWEZE KWENDA BRAZIL KOMBE LA DUNIA

..JUMANNE KESHO WAWILI GANI KATI YA GHANA, BURKINABE, EGYPT & ALGERIA KUTUA BRAZIL?

JUMANNE Usiku Timu mbili za mwisho, zitakazoungana na Nigeria, Ivory Coast na Cameroun, zitapatikana toka Bara la Afrika kwenda Brazil Mwakani Mwezi Juni kwenye Fainali za Kombe la Dunia na Egypt wanahitaji miujiza mikubwa ili kupindua kisago cha 6-1 ili wao waende Brazil badala ya Ghana.

AFRIKA
RATIBA
Marudiano
Jumanne Novemba 19
[Saa za Bongo]
[Katika Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
19:00 Egypt v Ghana [1-6]
21:15 Algeria v Burkina Faso [2-3]

EGYPT_v_GHANAKatika Mechi nyingine ya Jumanne Usiku, Burkina Faso, ambao walifungwa Fainali ya AFCON 2013 na Nigeria, wanatinga Algiers wakiwa na ushindi  wa 3-2 mbele ya Algeria walioupata katika Mechi ya kwanza.
Egypt watatua kwenye Mechi hii na Ghana itayochezwa Uwanja wa Jeshi Mjini Cairo wakiwa wamepata morali baada ya Klabu yao Al Ahly Wiki iliyopita kutwaa Ubingwa wa Afrika huku Gwiji wao Mohamed Aboutrika akifunga katika Mechi zote mbili dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Aboutrika ndie ataiongoza Egypt ikisaka miujiza mkubwa kwenye Soka wa kuibwaga Ghana na kufuta Bao 6-1.
Lakini Nahodha wa Ghana, Asamoah Gyan, ambae alifunga Bao 2 walipoichapa Misri 6-1 huko Kumasi Nchini Ghana, amekataa kuipuuza Misri.
Gyan ametamka: “Hii ni Soka na lolote linaweza kutokea!”
Aliongeza: “Tuko kwenye nafasi nzuri hivi sasa lakini lazima tutilie mkazo kwenye kazi yetu na kuhakikisha tunafika Brazil.”
Alhamisi iliyopita, Egypt iliifunga Zambia Bao 2-0 kwenye Mechi ya Kirafiki na Kocha wao toka Marekani, Bob Bradley, ameahidi kufanya mabadiliko kwenye Timu.
Awali Ghana waliitaka FIFA kutazama upya pambano hilo la Marudiano kuchezwa Mjini Cairo hasa kwa sababu za kiusalama lakini FIFA, baada ya kuhakikishiwa usalama na Serikali ya Egypt, imebariki Mechi hiyo kuchezwa Cairo.
Safari hii, Black Stars, kama inavyoitwa Ghana, itaimarika kwa kuwapata Nyota wao Kevin-Prince Boateng, alieikosa Mechi ya kwanza baada ya kuumia, na Harrison Afful, aliekuwa na Kadi, lakini upo wasiwasi wa kumkosa Beki David Addy ambae ana maumivu ya enka.

Baada ya Mechi hii ya Egypt na Ghana, huko Algiers, Algeria itacheza na Burkina Faso Uwanja wa Mustapha Tchaker huko Blida ambako Algeria hawajafungwa tangu 2002 na zimeshapita Mechi 19 hadi sasa.

Mwezi Juni, kwenye Uwanja huo huo, Algeria waliipiga Burkina Faso Bao 2-0 kwenye Mechi ya Kirafiki.
Kocha wa Algeria anaetoka Bosnia, Vahid Halihodzic, amedai walifungwa Bao 3-2 huko Ouagadougou katika Mechi ya kwanza kwa sababu ya upendeleo wa Marefa.
Burkinabe watatinga kwenye Mechi hii wakiwa wameimarika baada ya Straika wao hatari  Alain Traore, ambae aliikosa Mechi ya kwanza, kupona maumivu yake.

TIMU AMBAZO ZIMEFUZU KWENDA BRAZIL

[Jumla 24 Bado 8]:

Afika [Nchi 3 Bado 2]: Nigeria, Ivory Coast, Cameroun
Europe [Nchi 9 Bado 4]: Belgium, Bosnia-Herzegovina, England, Germany, Italy, Netherlands, Russia, Spain, Switzerland
South America [Nchi 5, Uruguay wapo kwenye Nchujo]: Argentina, Brazil (Wenyeji), Chile, Colombia, Ecuador
Asia [Nchi 4, Jordan wapo kwenye Mchujo]: Australia, Iran, Japan, South Korea

North & Central America/Caribbean [Nchi 3, Mexico wapo kwenye Mchujo]: Costa Rica, Honduras, USA

Oceania[New Zealand wapo kwenye Mchujo]

0 comments: