>>WENGER ANAAMINI GIROUD NI KIBOKO KUPITA ‘SAS’, SUAREZ & STURRIDGE!
>>CHELSEA KUFUNGUA JUMAMOSI ST JAMES PARK NA NEWCASTLE!!
>>MABINGWA MAN UNITED NDANI YA CRAVEN COTTAGE NA FULHAM!!
>>MAN CITY: KIPA JOE HART BENCHI…. PANTILIMON NAMBA 1!!
RATIBA
Jumamosi Novemba 2
[Saa za Bongo]
1545 Newcastle v Chelsea
1800 Fulham v Man Utd
1800 Hull v Sunderland
1800 Man City v Norwich
1800 Stoke v Southampton
1800 West Brom v Crystal Palace
1800 West Ham v Aston Villa
2030 Arsenal v Liverpool
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
BPL,
Ligi Kuu England, Jumamosi inaingia Mechi zake za 10 kwa Msimu huu na
Mechi 8 zitachezwa Jumamosi na mbili Jumapili lakini Mechi ya Jumamosi
Uwanjani Emirates kati ya Arsenal na Liverpool ndio BIGI MECHI.
Lakini habari kubwa huko England ni
uamuzi wa Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini kumbwaga Kipa wa
England Joe Hart na kuamua Kipa Nambari mbili Costel Pantilimon,
anaetoka Romania, kucheza Mechi yao ya Jumamosi na Norwich City Uwanjani
Etihad.
Joe Hart amekuwa akilaumiwa kwa makosa
makubwa na hasa Wikiendi iliyopita wakati yeye na Sentahafu wake Matija
Nastasić walipojichanganya na kumruhusu Fernando Torres kuifungia
Chelsea Bao la Pili na la ushindi Uwanjani Stamford Bridge Chelsea
walipoifunga Man City 2-1.
Nae Arsene Wenger, akikabiliwa na BIGI
MECHI ndani ya Emirates kati ya Timu yake Arsenal na Liverpool, ametoa
matumaini makubwa alipodai Sentafowadi wake Olivier Giroud ni
Sentafowadi wa uhakika kupita na Luis Suarez na mwenzake Daniel
Sturridge ambao hivi sasa kwenye Ligi Kuu England wamebatizwa jina ‘SAS’
likimaanisha kile Kikosi maalum cha Jeshi Uingereza cha Makomandoo
‘Special Air Services’.
Wenger aliwania kumnunua Luis Suarez kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa Septemba 2.
Suarez, ambae alichelewa kuanza kucheza
Mechi za Ligi Msimu huu akimalizia Kifungo chake cha Mechi 10 alichopewa
Mwezi Aprili kwa kumng’ata meno Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic,
Msimu huu kwenye Ligi amefunga Bao 6 katika Mechi 5.
Matumaini makubwa ya Arsenal kwa Magoli
ni Olivier Giroud ambae hadi sasa amecheka na nyavu mara 8 na Wenger
amesisitiza hilo aliposema: “Ikiwa Klabu zilitaka kumnunua Suarez ni
sababu ya kucheza vizuri lakini kwa sasa mie mkazo wangu ni Wachezaji wa
Arsenal. Naamini tangu Msimu huu uanze Giroud ni Straika wa kipekee na
atatimiza hilo kwenye Mechi hii. Yeye na Suarez wana staili tofauti
lakini Giroud ni Sentafowadi wa ukweli wakati Suarez ni mpiga chenga!”
Mechi za Ligi Wikiendi hii zitaanza
Jumamosi kwa Mechi ya mapema kabisa huko St James Park wakati Newcastle
watakapocheza na Chelsea.
Mabingwa Man United wapo Ugenini Craven Cottage kucheza na Fulham.
MECHI ZIJAZO:
BPL:LIGI KUU ENGLAND RATIBA [Saa za Bongo] Jumamosi Novemba 2 |
|
15:45 |
Newcastle v Chelsea |
18:00 |
Fulham v Man Utd |
18:00 |
Hull v Sunderland |
18:00 |
Man City v Norwich |
18:00 |
Stoke v Southampton |
18:00 |
West Brom v Crystal Palace |
18:00 |
West Ham v Aston Villa |
20:30 |
Arsenal v Liverpool |
Jumapili Novemba 3 |
|
13:30 |
Everton v Tottenham |
16:00 |
Cardiff v Swansea |
Jumamosi Novemba 9 |
|
18:00 |
Aston Villa v Cardiff |
18:00 |
Chelsea v West Brom |
18:00 |
Crystal Palace v Everton |
18:00 |
Liverpool v Fulham |
18:00 |
Southampton v Hull |
20:30 |
Norwich v West Ham |
Jumapili Novemba 10 |
|
15:00 |
Tottenham v Newcastle |
17:05 |
Sunderland v Man City |
19:10 |
Man Utd v Arsenal |
19:10 |
Swansea v Stoke |
Jumamosi Novemba 23 |
|
15:45 |
Everton v Liverpool |
18:00 |
Arsenal v Southampton |
18:00 |
Fulham v Swansea |
18:00 |
Hull v Crystal Palace |
18:00 |
Newcastle v Norwich |
18:00 |
Stoke v Sunderland |
20:30 |
West Ham v Chelsea |
Jumapili Novemba 24 |
|
16:30 |
Man City v Tottenham |
19:00 |
Cardiff v Man Utd |
Jumatatu Novemba 25 |
|
23:00 |
West Brom v Aston Villa |
Jumamosi Novemba 30 |
|
18:00 |
Aston Villa v Sunderland |
18:00 |
Cardiff v Arsenal |
18:00 |
Everton v Stoke |
18:00 |
Norwich v Crystal Palace |
18:00 |
West Ham v Fulham |
20:30 |
Newcastle v West Brom |
Jumapili Desemba 1 |
|
15:00 |
Tottenham v Man Utd |
17:05 |
Hull v Liverpool |
19:10 |
Chelsea v Southampton |
19:10 |
Man City v Swansea |
Jumanne Desemba 3 |
|
20:00 |
Crystal Palace v West Ham |
Jumatano Desemba 4 |
|
22:45 |
Arsenal v Hull |
22:45 |
Liverpool v Norwich |
22:45 |
Man Utd v Everton |
22:45 |
Southampton v Aston Villa |
22:45 |
Stoke v Cardiff |
22:45 |
Sunderland v Chelsea |
22:45 |
Swansea v Newcastle |
23:00 |
Fulham v Tottenham |
23:00 |
West Brom v Man City |
0 comments:
Post a Comment