Hatimaye
Yanga wamefanikiwa kuwapiku Simba katika uongozi wa kinyang'anyiro cha
"Nani Mtani Jembe?" baada ya kuchukua uongozi ambao ulishikiliwa na
Simba tangu kampeni ilipoanza. Yanga ambao pia ni ni vinara wa ligi kuu
hivi sasa wana jumla ya Sh. 56,580,000.00 huku Simba wakiwa na Sh.
43,420,000.00.
Kampeni ya "Nani Mtani Jembe?" inaendeshwa na Kilimanjaro Premium Lager ambayo imetoa jumla ya Shilingi milioni 100 zilizogawiwa nusu kwa Simba na Yanga huku mashabiki wakitakiwa kuziwezesha timu zao kupata kitita kikubwa zaidi kwa kutuma namba zilizo chini ya kizibo cha bia ya Kilimanjaro kwenda 15440 ambapo shilingi 1000 hukatwa toka kwa wapinzani na kuongezwa kwa timu wanayoshabikia. Kampeni ya "Nani Mtani Jembe?" inatarajiwa kuhitimishwa Desemba 14 kwa mpambano wa Yanga na Simba uwanja wa taifa ambapo timu zote zitakabidhiwa kitita zilichojipatia.

Source wavutiblog
0 comments:
Post a Comment