>>YAFUNGWA 2-1 MJINI CAIRO, YAPITA JUMLA BAO 7-3!!
GHANA Usiku huu imekuwa Nchi ya 4 toka
Afrika, baada ya Nigeria, Ivory Coast na Cameroun, kufuzu kucheza
Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwezi Juni Mwakani licha ya
kufungwa Bao 2-1 Mjini Cairo na Egypt.
Ghana walishinda Mechi ya kwanza huko Kumasi Mwezi uliopita kwa Bao 6-1 na hivyo wamefuzu kwa Jumla ya Mabao 7-3.
AFRIKA
RATIBA/MATOKEO:
Marudiano
Jumanne Novemba 19
Egypt 2 Ghana 1 [Jumla ya Mabao Mechi mbili 3-7]
[Saa za Bongo]
[Katika Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
21:15 Algeria v Burkina Faso [2-3]
Egypt
ndio walitangulia kupata Bao 2, Bao moja kila Kipindi, kwa Bao za Amr
Zaky, baada frikiki ya Gwiji Mohamed Aboutrika, na Bao la pili kupitia
Mohamed Nagy-Gedo.
Bao la Ghana lilifungwa na Kevin Prince Boateng alieingia Kipindi cha Pili.
Baadae leo Timu ya 5 na ya mwisho kwa
Afrika kwenda Fainali za Kombe la Dunia itajulikana baada ya Mechi ya
huko Mjini Algiers kati ya Algeria na Burkina Faso ambapo Burkina Faso
wako mbele kwa Bao 3-2 waliposhinda Mechi ya kwanza.
VIKOSI:
EGYPT: Sherif Ekrami –
Hazem Emam, Rami Rabiea, Mohamed Naguib, Mohamed Abdel-Shafy – Hossam
Ghaly, Ahmed Fathi – Mahmoud Abdel-Moneim 'Kaharaba', Mohamed
Abou-Treika, Mohamad Salah, Amr Zaki.
GHANA: Fatau Dauda -
Harrison Afful, Daniel Opare, Jerry Akaminko, Rashid Sumaila - Michael
Essien, Andre Ayew, Sulley Muntari, Kwadwo Asamoah - Abdul Majeed Waris,
Asamoah Gyan.
Refa: Noumandiez DOUE (Ivory Coast)
TIMU AMBAZO ZIMEFUZU KWENDA BRAZIL
[Jumla 25 Bado 7]:
Afika [Nchi 4 Bado 1]: Nigeria, Ivory Coast, Cameroun, Ghana
Europe [Nchi 9 Bado 4]: Belgium, Bosnia-Herzegovina, England, Germany, Italy, Netherlands, Russia, Spain, Switzerland
South America [Nchi 5, Uruguay wapo kwenye Nchujo]: Argentina, Brazil (Wenyeji), Chile, Colombia, Ecuador
Asia [Nchi 4, Jordan wapo kwenye Mchujo]: Australia, Iran, Japan, South Korea
North & Central America/Caribbean [Nchi 3, Mexico wapo kwenye Mchujo]: Costa Rica, Honduras, USA
Oceania[New Zealand wapo kwenye Mchujo]
0 comments:
Post a Comment