UWANJA: BayArena JIJINI: Leverkusen SAA: 22:45
LEO USIKU huko Germany ipo Mechi ya
Marudiano ya Kundi A la UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, kati ya Bayer
Leverkusen na Manchester United.
Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa Old Trafford Mwezi Septemba, Man United iliifunga Bayer Leverkusen Bao 4-2.
Katika Mechi ya leo, Man United
wanahitaji ushindi ili wafuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL
lakini pia hata Sare itawafanikisha.
MSIMAMO:
KUNDI A |
|||||||||
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
1 |
Manchester United |
4 |
2 |
2 |
0 |
6 |
3 |
3 |
8 |
2 |
Bayer 04 Leverkusen |
4 |
2 |
1 |
1 |
8 |
5 |
3 |
7 |
3 |
FC Shakhtar Donetsk |
4 |
1 |
2 |
1 |
3 |
5 |
-2 |
5 |
4 |
Real Sociedad |
4 |
0 |
1 |
3 |
1 |
5 |
-4 |
1 |
Lakini,
Bayer Leverkusen, ambao Meneja wao ni Mchezaji wa zamani wa Liverpool,
Sami Hyypia, hivi sasa wamegangamala na tangu wafungwe 4-2 na Man United
wamepoteza Mechi 1 tu katika Mechi 12 na kwenye Bundesliga wapo Nafasi
ya Pili nyuma ya Bayern Munich.
Vile vile, Uwanjani kwao BayArena hawafungiki na mara ya mwisho kufungwa ni Mwezi walipofungwa na Mabingwa Bayern Munich.
Hali za Wachezaji
Marouane Fellaini ataikosa Mechi hii
baada ya kupewa Kadi Nyekundu walipotoka 0-0 na Real Sociedad katika
Mechi iliyopita ya Kundi A la UCL.
Wengine ambao hawakusafiri kwenda
Germany kwa sababu wana maumivu ni Michael Carrick, Nemanja Vidic na
Robin van Persie lakini Rafael na Phil Jones waliokuwa majeruhi wamo
kwenye Kikosi kilichosafiri.
Bayer Leverkusen watamkosa Sidney Sam
ambae amewafungia Bao 8 Msimu huu baada kuumia walipocheza na Hertha
Berlin Mechi iliyopita na pia upo wasiwasi kuhusu Beki wao Sebastian
Boenisch ambae ana maumivu.
Katika Mechi iliyopita kati ya Man
United na Bayer Leverkusen, Bao za Man United zilifungwa na Wayne
Rooney, Bao 2, Robin van Persie na Antonio Valencia huku Bao la Bayer
Leverkusen likifungwa na Simon Rolfes.
VIKOSI VINATARAJIWA:
BAYER LEVERKUSEN: Leno; Donati, Toprak, Wollscheid, Can; Rolfes, Bender, Castro; Son, Kießling, Hegeler
MAN UNITED: De Gea; Smalling, Ferdinand, Evans, Evra; Cleverley, Giggs; Valencia, Rooney, Januzaj; Welbeck
REFA: Svein Oddvar Moen [Norway]
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RATIBA:
[Mechi zote kuanza Saa 22:45 isipokuwa inapotajwa]
Jumatano 27 Novemba 2013
Bayer 04 Leverkusen v Manchester United FC
FC Shakhtar Donetsk v Real Sociedad de Fútbol
Real Madrid CF v Galatasaray A.Åž.
Juventus v FC København
RSC Anderlecht v SL Benfica
Paris Saint-Germain v Olympiacos FC
PFC CSKA Moskva v FC Bayern München [20:00]
Manchester City FC v FC Viktoria Plzeň
0 comments:
Post a Comment