KWA MUHUTASALI
ZIJUE KAMATI NDONGONDOGO ZA TFF!
RAGE AAGIZWA KUITISHA MKUTANO SIMBA NDANI YA SIKU 14!!
PATA TAARIFA KAMILI ZA TFF:
Release No. 009
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Novemba 24, 2013
KILIMANJARO STARS KUAGWA KESHO
Kikosi cha Kilimanjaro Stars kinaagwa
kesho (Novemba 25 mwaka huu) tayari kwa safari ya Nairobi, Kenya
kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza kutimua vumbi Novemba
27 mwaka huu.
Hafla ya kuiaga timu hiyo itafanyika saa
5 asubuhi kambini kwao katika hoteli ya Accomondia jijini Dar es
Salaam. Msafara wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager utaongozwa na Ahmed Idd Mgoyi. Timu itaondoka saa 10
alasiri kwa ndege ya RwandAir.
Wachezaji waliomo katika msafara huo ni
makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na
Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam),
Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu
Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman
Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan
Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar
(Azam).
Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias
Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma
Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa
(Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Hata hivyo, washambuliaji Samata na
Ulimwengu watajiunga na timu hiyo jijini Nairobi, Desemba Mosi mwaka huu
wakitokea Lubumbashi ambapo Novemba 30 mwaka huu TP Mazembe itacheza
fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Benchi la Ufundi la timu hiyo
linawajumuisha Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha
Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa Makipa), Leopold Tasso (Meneja wa
Timu), Dk Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa Timu), Frank Mhonda (mtaalamu
wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza Vifaa).
Kilimanjaro Stars ambayo ipo kundi B
katika michuano hiyo itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka
dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Release No. 200
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Novemba 23, 2013
TFF YAUNDA KAMATI NDONGONDOGO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametangaza wajumbe wa kamati ndogongo
(standing committees) wakati zile za haki (judicial organs) na uchaguzi
zitaundwa baadaye.
Akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika leo (Novemba 23
mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Rais Malinzi alisema kamati hizo
zimeundwa kwa mujibu wa katiba ili kuisaidia Kamati ya Utendaji.
Pia ametangaza wajumbe wanne wa Kamati
ya Utendaji aliowateua. Wajumbe hao ni Richard Sinamtwa na Ramadhan
Nassib, wakati wengine wanaoingia moja kwa moja kwenye Kamati ya
Utendaji kutokana na kamati wanazoziongoza ni Dk. Paul Marealle na
Saloum Umande Chama.
Kamati ya Fedha na Mipango inaongozwa na
Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wajumbe ni Francis Ndulane
(Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammed, Geofrey
Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian Kuhyava.
Geofrey Nyange anaongoza Kamati ya
Mashindano wakati wajumbe ni Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri
Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed,
Gerald ambi, Davis Mosha, Said George na Nassoro Idrissa.
Kinara wa Kamati ya Ufundi ni Kidao
Wilfred wakati wajumbe ni Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedstus
Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin,
Nicholas Mihayo na Dk. Cyprian Maro.
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana
inaongozwa na Ayoub Nyenzi, Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali
Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali
Charles Mbuge, Lameck Nyambaya na Ibrahim Masoud.
Lina Kessy anaongoza Kamati ya Mpira wa
Miguu wa Wanawake wakati wajumbe ni Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti),
Zena Chande, Amima Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder,
Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o na Engrid Kimaro.
Kamati ya Waamuzi inaongozwa na Saloum
Umande Chama, Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala
(Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor
Mwandike, Soud Abdi na Zahra Mohamed.
Hamad Yahya Juma ambaye ni Mwenyekiti wa
Bodi ya Ligi anaongoza Kamati ya Habari na Masoko wakati wajumbe ni
Naibu Waziri January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf
Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela
na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA).
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji
inaongozwa na Richard Sinaitwa, Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti),
Zacharia Hanspoppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko na
Imani Madega.
Kiongozi wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha
ni Ramadhan Nassib wakati wajumbe ni Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti),
Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson,
Goodluck Moshi, Golden Sanga na Elias Mwanjala.
Dk. Paul Marealle anaongoza Kamati ya
Tiba wakati wajumbe ni Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk.
Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema na Asha
Sadick.
RAGE AAGIZWA KUITISHA MKUTANO SIMBA
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage ameagizwa kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wa klabu ndani ya siku 14 kuanzia sasa.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa mgogoro katika klabu
baada ya kupokea barua mbili; moja kutoka Kamati ya Utendaji ikielezea
kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti huyo
ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.
Uamuzi wa TFF umefanywa kwa kuzingatia
Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba inayosema: “Simba Sports Club ni
mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF
na FIFA, na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake.”
TFF itatuma wawakilishi wake katika
mkutano huo, na kumuagiza Mwenyekiti wa Simba kuhakikisha wanachama wote
wenye hoja wanapata fursa ya kusikilizwa.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment