Leo asubuhi zilitoka taarifa kwamba klabu ya Simba kupitia kamati ya utendaji imemsimamisha Mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage kutokana na kamati hiyo kukosa imani nae juu ya utendaji wake.
Muda mfupi baada ya
kusimamishwa kwa Rage, viongozi wa klabu hiyo waliandaa mkutano wa
waandishi wa habari ambapo pia makocha Abdallah 'King' Kibaden na
Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ wameondolewa kwenye timu na nafasi
yao itachukuliwa na aliyekuwa kocha Gor Mahia ya Kenya Zdravko Logarusic atakayetambulishwa Desemba 1, mwaka huu akisaidiwa na kocha wa timu B Selemani Matola.
Kuhusu Rage, kaimu
makamu mwenyekiti wa Simba Mzee Kinesi amesema kwamba uongozi umekosa
imani na Rage na hivyo walikaa kikao jana na kufikia maamuzi ya
kumsimamisha, pia hawajaridhishwa na ufundishaji wa Julio na Kibaden
ndio maana wanawaondoa. Rage ambaye hakuwepo katika kikao cha jana
nafasi yake itakaimiwa na Mzee Kinesi sasa mpaka hapo mbele
utakapochukuliwa uamuzi mwingine.
0 comments:
Post a Comment