Wednesday 20 November 2013

RAIA WATATU 3 WA EAC WAIPEREKA COW KWENYE MAHAKAMA YA HAKI YA AFRIKA

Raia watatu kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamefungua ombi katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki siku ya Jumatatu (tarehe 18 Novemba) kwamba "Muungano wa Waliotayari" (Coalition of the Willing) yaani Kenya, Rwanda na Uganda ziadhibiwe kwa kuendesha mikutano ya kikanda bila ya wanachama wa mataifa wenzao ya EAC ya Tanzania na Burundi.

Ally Msangi, David Mataka, na John Adam Bwenda walifungua ombi lao kwa Jimmy Obed Advocates mjini Dar es Salaam, na 
Jimmy Obed akitajwa pia kuwa ni mwombaji, gazeti la The Guardian la Tanzania liliripoti siku ya Jumanne.

Obed aliitaka mahakama kutoa onyo kwa Kenya, Rwanda na Uganda kwa kuhatarisha mahusiano ndani ya umoja wa EAC. Aliongeza kwamba malalamiko rasmi yalikusudiwa kufikishwa mahakamani ili kuchapisha taarifa ya kuyataka mataifa wanachama wa EAC kulinda itifaki ya umoja huo wa biashara ya kikanda.

"Kama raia wa EAC tunayo haki ya kuitaka mahakama kufanyia kazi maombi yetu na kutoa amri ambayo itakataza utekelezaji wa makubaliano ya kile kilichofikiwa katika mikutano hiyo 'kinyume na sheria' na nchi tatu hizo" Obed alisema.

Wanaharakati hao wanadai kuwa mikutano hiyo ya kanda inakiuka vifungu kadhaa na sheria za mkataba wa EAC. ---  
 

 

0 comments: