>>BAYERN,MAN CITY, ATLETICO, BARCA WAMESHAPITA, NANI KUUNGANA?
WAKATI
Manchester City, Bayern Munich, Atlético Madrid na Barcelona
zimeshafuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 huku wamebakisha Mechi
mbili mkononi za Makundi yao, Jumanne Novemba 26 Mechi za Tano za
Makundi zitaanza na ifuatayo ni tathmini ya Kundi kwa Kundi kujua nani
wngine wanaweza kufuzu.
KUNDI A
Bayer 04 Leverkusen (Pointi 7) v Manchester United FC (8)
FC Shakhtar Donetsk (5) v Real Sociedad de Fútbol (1)
Baada Mechi 4, ni Man United pekee ndio wenye uhakika wa kucheza Ulaya [CHAMPIONZ LIGI au EUROPA LIGI].
Man United wanaweza kutwaa Nafasi ya
Kwanza ya Kundi wakiifunga Bayer Leverkusen na Shakhtar Donetsk
kushindwa kuifunga Real Sociedad.
Bayer Leverkusen wanaweza kufuzu ikiwa wataifunga Man United.
Shakhtar wataendelea kuwa na matumaini ya kufuzu labda wafungwe na Mechi ya Leverkusen na Man United imalizike Sare.
Ili wabakie na matumaini kidogo ya kufuzu, Real Sociedad ni lazima washinde na kuomba Man United pia ishinde.
KUNDI B
Juventus (Pointi 3) v FC København (4)
Real Madrid CF (10) v Galatasaray AŞ (4)
Wakiwa wanaongoza kwa Pointi 6, Real
Madrid wanahitaji Sare tu watakapocheza Nyumbani kwao dhidi ya
Galatasaray ili watawe Nafasi ya Mshindi wa Kwanza wa Kundi lao na
kufuzu kwenda Raundi ya Mtoano.
Juventus, ambao hawajashinda hata Mechi
moja kwenye Kundi hili, watakwea Nafasi ya Pili wakiifunga FC København
na watafanikiwa kutwaa Nafasi ya Pili ikiwa pia wataifunga Galatasaray
Ugenini katika Mechi yao ya mwisho.
Lakini ikiwa Juve watafungwa na FC København basi watatupwa nje ya Mashindano haya.
KUNDI C
RSC Anderlecht (Pointi 1) v SL Benfica (4)
Paris Saint-Germain (10) v Olympiacos FC (7)
PSG wanahitaji Sare tu ili kushinda
Nafasi ya Mshindi wa Kwanza wa Kundi lao watakapocheza na Olympiacos
Timu ambayo waliitwanga Bao 4-1 huko Piraeus katika Mechi ya Kwanza ya
Kundi.
Olympiacos wanaweza kufuzu ikiwa watapata Sare na PSG huku Benfica wakishindwa kuifunga Anderlecht.
Benfica wanahitaji ushindi ili wabaki
kwenye kinyang’anyiro wakati Anderlecht wapo Mguu nje kwani wanahitaji
kushinda Mechi zote mbili zilizobakia na matokeo mengine yawasaidie wao.
KUNDI D
PFC CSKA Moskva (Pointi 3) v FC Bayern München (12)
Manchester City FC (9) v FC Viktoria Plzeň (0)
Bayern na Manchester City zimeshafuzu
kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na kuziacha CSKA na Plzeň kugombea
nafasi ya Tatu ili kucheza EUROPA LIGI.
Bayern watatwaa ushindi wa Kwanza wa Kundi hili ikiwa watapata matokeo bora kuliko Man City kwenye Mechi zao.
KUNDI E
FC Basel 1893 (Pointi 5) v Chelsea FC (9)
FC Steaua Bucureşti (2) v FC Schalke 04 (6)
Sare itawafanya Chelsea wafuzu na
wakishinda basi watatwaa Nafasi ya Kwanza ya Kundi na hata wakifungwa
Mechi hii na Basel ambayo pia iliwafunga 2-1 huko Stamford Bridge katika
Mechi ya Kwanza hakutawang’oa Chelsea toka kileleni mwa Kundi.
Schalke, ambao wako Nafasi ya Pili, wanaweza kufuzu tu ikiwa wao watashinda na Chelsea kushinda.
Ili wabakishe matumaini yao finyu, Steau Bucharest ni lazima washinde.
KUNDI F
Arsenal FC (Pointi 9) v Olympique de Marseille (0)
Borussia Dortmund (6) v SSC Napoli (9)
Marseille tayari wako nje lakini Arsenal
hawatafuzu hata wakishinda labda tu Borussia Dortmund, ambao wako
Nyumbani, washindwe kuifunga Napoli.
Ikiwa Arsenal watashinda na Dortmund kushindwa kuifunga Napoli, basi Dortmund watatupwa kwenye EUROPA LIGI.
Napoli watafuzu wakiifunga Dortmund na hilo pia litawafanya Arsenal wafuzu labda wafungwe na Marseille.
KUNDI G
FC Porto (Pointi 4) v FK Austria Wien (1)
FC Zenit (5) v Club Atlético de Madrid (12)
Atlético, ambao wana Pointi zote 12
baada kushinda Mechi zao za Kundi, ndio Timu pekee kwenye UEFA CHAMPIONZ
LIGI ambayo tayari imetwaa ushindi wa Kwanza wa Kundi.
Austrian Wien, ambao hawajafunga hata
Bao moja kwenye Kundi hili, wanahitaji kulifunika pengo la Pointi 4 toka
kwa Timu ya Pili Zenit.
Ikiwa Atletico watfungwa huko in St Petersburg, Porto ni lazima washinde ili kujiwekea uhai katika Mechi ya mwisho.
KUNDI H
AFC Ajax (Pointi 4) v FC Barcelona (10)
Celtic FC (3) v AC Milan (5)
Barcelona tayari wametinga Raundi ya
Mtoano ya Timu 16 na wakipata Sare huko Amsterdam wakicheza na Ajax
watatwaa Nafasi ya Kwanza ya Kundi.
Celtic watatwaa Nafasi ya Pili wakiifunga AC Milan na Ajax kushindwa kuifunga Barca.
Lakini Celtic wakifungwa tu wako nje ya Mashindano.
Ajax watashika Nafasi ya Pili wakiifunga Barca ikiwa AC Milan haitashinda.
Ikiwa Barca na AC Milan zote zitashinda Ugenini basi AC Milan itaungana na Barca kucheza Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RATIBA:
[Mechi zote kuanza Saa 22:45 isipokuwa inapotajwa]
Jumanne 26 Novemba 2013
FC Steaua Bucureşti v FC Schalke 04
FC Basel 1893 v Chelsea FC
Arsenal FC v Olympique de Marseille
Borussia Dortmund v SSC Napoli
FC Porto v FK Austria Wien
Football Club Zenit v Club Atlético de Madrid [20:00]
Celtic FC v AC Milan
AFC Ajax v FC Barcelona
Jumatano 27 Novemba 2013
Bayer 04 Leverkusen v Manchester United FC
FC Shakhtar Donetsk v Real Sociedad de Fútbol
Real Madrid CF v Galatasaray A.Ş.
Juventus v FC København
RSC Anderlecht v SL Benfica
Paris Saint-Germain v Olympiacos FC
PFC CSKA Moskva v FC Bayern München [20:00]
Manchester City FC v FC Viktoria Plzeň
MSIMAMO:
KUNDI A | |
|
|
|
|
|
|
|
|
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Manchester United | 4 | 2 | 2 | 0 | 6 | 3 | 3 | 8 |
2 | Bayer 04 Leverkusen | 4 | 2 | 1 | 1 | 8 | 5 | 3 | 7 |
3 | FC Shakhtar Donetsk | 4 | 1 | 2 | 1 | 3 | 5 | -2 | 5 |
4 | Real Sociedad | 4 | 0 | 1 | 3 | 1 | 5 | -4 | 1 |
KUNDI B | |
|
|
|
|
|
|
|
|
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Real Madrid CF | 4 | 3 | 1 | 0 | 14 | 4 | 10 | 10 |
2 | Galatasaray Spor Kulübü | 4 | 1 | 1 | 2 | 6 | 10 | -4 | 4 |
3 | FC Copenhagen | 4 | 1 | 1 | 2 | 3 | 8 | -5 | 4 |
4 | Juventus | 4 | 0 | 3 | 1 | 6 | 7 | -1 | 3 |
KUNDI C | |
|
|
|
|
|
|
|
|
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Paris Saint-Germain | 4 | 3 | 1 | 0 | 13 | 2 | 11 | 10 |
2 | Olympiacos CFP | 4 | 2 | 1 | 1 | 6 | 5 | 1 | 7 |
3 | Benfica | 4 | 1 | 1 | 2 | 3 | 5 | -2 | 4 |
4 | RSC Anderlecht | 4 | 0 | 1 | 3 | 1 | 11 | -10 | 1 |
KUNDI D | |
|
|
|
|
|
|
|
|
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Bayern Munich | 4 | 4 | 0 | 0 | 12 | 1 | 11 | 12 |
2 | Manchester City | 4 | 3 | 0 | 1 | 11 | 6 | 5 | 9 |
3 | CSKA Moskva | 4 | 1 | 0 | 2 | 6 | 12 | -6 | 3 |
4 | FC Viktoria Plzen | 4 | 0 | 0 | 4 | 3 | 12 | -9 | 0 |
KUNDI E | |
|
|
|
|
|
|
|
|
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Chelsea FC | 4 | 3 | 0 | 1 | 11 | 2 | 9 | 9 |
2 | Schalke | 4 | 2 | 0 | 2 | 4 | 6 | -2 | 6 |
3 | FC Basel 1893 | 4 | 1 | 2 | 1 | 4 | 4 | 0 | 5 |
4 | FC Steaua Bucuresti | 4 | 0 | 2 | 2 | 2 | 9 | -7 | 2 |
KUNDI F | |
|
|
|
|
|
|
|
|
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Arsenal | 4 | 3 | 0 | 1 | 6 | 3 | 3 | 9 |
2 | Napoli | 4 | 3 | 0 | 1 | 7 | 6 | 1 | 9 |
3 | BV Borussia Dortmund | 4 | 2 | 0 | 2 | 6 | 4 | 2 | 6 |
4 | Olympique de Marseille | 4 | 0 | 0 | 4 | 4 | 10 | -6 | 0 |
KUNDI G | |
|
|
|
|
|
|
|
|
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Atletico de Madrid | 3 | 3 | 0 | 0 | 8 | 2 | 6 | 12 |
2 | Zenit St. Petersburg | 4 | 1 | 2 | 1 | 3 | 4 | -1 | 5 |
3 | FC Porto | 4 | 1 | 1 | 2 | 3 | 4 | -1 | 4 |
4 | FK Austria Wien | 4 | 0 | 1 | 3 | 0 | 8 | -8 | 1 |
KUNDI H | |
|
|
|
|
|
|
|
|
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | FC Barcelona | 4 | 3 | 1 | 0 | 9 | 2 | 7 | 10 |
2 | AC Milan | 4 | 1 | 2 | 0 | 5 | 5 | 0 | 5 |
4 | Ajax Amsterdam | 4 | 1 | 1 | 2 | 3 | 7 | -4 | 4 |
3 | Celtic | 4 | 1 | 0 | 2 | 2 | 4 | -2 | 3 |
MECHI ZA MWISHO ZA MAKUNDI
Jumanne 10 Desemba 2013
Manchester United FC v FC Shakhtar Donetsk
Real Sociedad de Fútbol v Bayer 04 Leverkusen
Galatasaray v A.Ş. Juventus
FC København v Real Madrid CF
SL Benfica v Paris Saint-Germain
Olympiacos v FC RSC Anderlecht
FC Bayern München v Manchester City FC
FC Viktoria Plzeň v PFC CSKA Moskva
Jumatano 11 Desemba 2013
FC Schalke 04 v FC Basel 1893
Chelsea FC v FC Steaua Bucureşti
Olympique de Marseille v Borussia Dortmund
SSC Napoli v Arsenal FC
FK Austria Wien v Football Club Zenit
Club Atlético de Madrid v FC Porto
AC Milan v AFC Ajax
FC Barcelona v Celtic FC
0 comments:
Post a Comment