Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amemshitaki mmoja wa viongozi wa CHADEMA polisi.
Habari zimedai kuwa Zitto amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.
Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la

Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.
Hata hivyo, Kibatara hakusema waraka huo unasema nini, na kwa nini hali hiyo inatokea kwa sasa katika kipindi ambacho Zitto anakabiliwa na tuhuma za usaliti ndani ya chama chake.
Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima Jumatano, Kileo alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto: “Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine,” alisema Kileo.
Zitto kutwa nzima ya jana hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kufafanua mashitaka aliyofungua polisi. Simu zake zote za kiganjani zilikuwa zimezimwa.
via gazeti la TanzaniaDaima

0 comments:
Post a Comment