Sunday 17 November 2013

IVORY COAST NA MABINGWA AFRIKA NIGERIA, KUTUA BRAZIL KATIKA KOMBE LA DUNIA

.....IVORY COAST WATOA SARE NA SENEGAL 1-1
...... NIGERIA WAICHAPA ETHIPIA BAO 2-0

JANA Usiku huko Casablanca, Morocco, Ivory Coast imefanikiwa kuungana na Mabingwa wa Afrika, Nigeria, na kuwa Nchi za kwanza toka Afrika kutinga kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwakani baada ya kutoka Sare 1-1 na Senegal na kupita kwa Jumla ya Mabao 4-2.
Ivory Coast waliifunga Senegal Bao 3-1 katika Mechi ya kwanza iliyochezwa Mjini Abidjan Mwezi Oktoba.

VIKOSI VILIVYOANZA SENEGAL NA IVORY COAST:
SENEGAL: Bouna Coundoul: Idrissa Gueye, Kara Mbodji, Lamine Sane, Pape Souare, Papy Djilobodji, Sadio Mane, Salif Sane, Stephane Badji, Dame Ndoye, Papiss Cisse
IVORY COAST: Boubacar Barry, Jean Jacques Gosso, Kolo Toure, Sol Bamba, Serge Aurier, Yaya Toure, Didier Zokora, Romaric, Gervinho, Salomon Kalou, Dider Drogba
.
 na
MABINGWA wa Afrika, Nigeria, wali hapo Jana huko kwao UJ Esuene Stadium Mjini Calabar, wameichapaSTEPHEN_KESHIEthiopia Bao 2-0 na kuwa Nchi ya kwanza toka Bara la Afrika kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwakani.
Afrika inazo Nafasi 5 kwenye Fainali za Kombe la Dunia na nyingine zitaamuliwa baada ya Mechi nyingine 4 za Marudiano za Raundi ya Mwisho ambazo zinaendelea leo, kesho na Jumanne.

Jana Nigeria, ambao waliifunga Ethiopia Bao 2-1 huko Addis Ababa katika Mechi ya kwanza Mwezi Oktoba, walifunga kupitia Victor Moses, Penati ya Dakika ya 20, na Mchezaji alietoka Benchi, Victor Obinna, kwa frikiki ya Dakika ya 83.
Hii itakuwa mara ya 5 kwa Nigeria kucheza Fainali za Kombe la Dunia.

VIKOSI VILIVYOANZA: NIGERIA NA ETHIOPIA
NIGERIA: Vincent Enyeama, Godfrey Oboabona, Uwa Echiejile, Efe Ambrose, Ahmed Musa, Ideye Brown, Emmanuel Emenike, John Mikel Obi, Victor Moses, Ogenyi Onazi, Kenneth Omeruo
ETHIOPIA: Sisay Bancha, Alula Girma, Asrat Gobena, Aynalem Hailu, Bargicho Salahadin, Butako Abebaw, Getaneh Gibeto, Girma Adane, Minyahile Beyene, Salahdin Ahmed, Shemeles Bekele


AFRIKA
RATIBA/MATOKEO:

Jumamosi Novemba 16
Nigeria 2 Ethiopia 0 [Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili 4-1]
Senegal 1 Ivory Coast 1 [Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili 2-4]
[Saa za Bongo]
[Katika Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Jumapili Novemba 17
17:30 Cameroon v Tunisia [0-0]
Jumanne Novemba 19
19:00 Egypt v Ghana [1-6]
21:15 Algeria v Burkina Faso [2-3]
 FAHAMU: Washindi 5 ndio watacheza Fainali za Kombe la Dunia na  bado timu 3 tatu kutinga Brazil

0 comments: