
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh Abbas Kandoro mara baada ya kuwasili katika ofisi za chama hicho mjini Vwawa Wilaya ya Mbozi asubuhi hii akitokea wilaya ya Momba katika ziara yake ya kikazi ya mikoa mitatu Ruvuma, Mbeya na Njombe, Kinana ameongozana na ujumbe wake akiwa na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MBOZI
Dr.
Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro mara baada ya
msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ku wasili mjini Vwawa wilayani Mbozi
asubuhi hii, kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na
Uenezi
Baadhi
ya wana CCM wakishiriki kucheza ngoma na kikundi cha ngoma kilichokuwa
kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana.(P.T)
Baadhi ya machifu wa Mbozi wakisubiri kusalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Baadhi
ya viongozi mbalimbali na wananchi wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana wakati alipowasili wilayani Mbozi.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Mbeya na mbunge wa jimbo la Mbozi mashariki Ndugu
Godfrey Zambi akisalimiana na wana CCM wakati wa mapokezi hayo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na machifu
Wana CCM wakiwa katika mapokezi hayo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifutrahia ngoma ya asili ya wanyiha iliyokuwa ikitumbuizwa katika mapokezi hayo.
- Imeandikwa Na Mjengwa Blog












0 comments:
Post a Comment