Tuesday 19 November 2013

MECHI YA KIRAFIKI: TANZANIA, ZIMBABWE WATOKA 0-0!

>>STARS: KIKOSI KAMILI, MAPROFESHENALI TOKA NJE!!
>>MASHABIKI WAGOMA KUKUBALI ZIMBABWE IPO 102, SISI 129 UBORA DUNIANI, WALIA KUTOSHINDA, WAMZOMEA KIM!!

TAIFA_STARS-BORA1Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam hii leo kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania na ile ya Zimbabwe ilimalizika kwa Sare ya 0-0.
Mechi hii, ambayo imechezwa kwenye Siku ya Kalenda ya FIFA, ilisaidia Kikosi cha Tanzania kuwachezesha Wachezaji wao kadhaa ambao ni Maprofeshenali wanaocheza nje ya Nchi ambao ni Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaocheza huko Congo DR kwenye Klabu ya TP Mazembe, Mwinyi Kazimoto anaicheza Klabu ya Qatar Al-Markhiya Sports Club na Shomari Kapombe wa AS Cannes ya huko France.

Hata hivyo Kikosi hicho kilishindwa kung’ara na kufifia kadiri Mechi ilivyoendelea na kuwafadhaisha Mashabiki waliojaa Uwanjani ambao walikataa kukubali Zimbabwe ni Timu nzuri iliyo Nafasi ya 102 kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani ukilinganisha Tanzania ambayo iko Nafasi ya 129.
Hali hiyo ilisababisha baadhi ya Mashabiki kumzomea Kocha wa Taifa Kim Poulsen.

VIKOSI:
TANZANIA: Ivo Mapunda, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni [Himid Mao, 56], Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Hassan Dilunga [Salum Abubakar, 51], Mwinyi Kazimoto [Amri Kiemba, 51], Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa [Farid Musa, 80].
ZIMBABWE: Tapiwa Kapini, Ocean Mushere, Carrington Nyandemba, Obey Mureneheri, Themba Ndhlovu, Isaac Majari, Kapinda Wonder, Kundawashe Mahachi, Warren Dube, Lot Chiungwa, Simba Sithole.
REFA: Ronnie Kalema [Uganda]

0 comments: