Manchester
United jana nusura wapate ajali kama iliyowahi kuwakumba miaka kadhaa
iliyopita huko Munich baada ya ndege waliyopanda kusitisha zoezi la
kutua mita 400 kutoka kwenye sehemu ya kutulia ndege kwenye uwanja wa Konrad Adenauer uliopo huko Cologne Ujerumani.
Ndege
ya shirika la Monarch Airlines A321, namba MON 9254, ilipangwa kutua
uwanjani hapo 5.30pm kwa muda wa Ujerumani, lakini rubani alilazimika
kusitisha kutua kwa ndege hiyo kwa sababu kulikuwa na ndege nyingine
kwenye sehemu ya kutulia. Ndege hiyo waliyopanda United ikabidi izunguke
uwanja hewani na kuja kutua dakika 10 baadae saa 5.40pm.
Abiria
mmoja katika ndege hiyo, ambayo ilikuwa na wachezaji wote wa United na
maofisa wengine wa timu hiyo akiwemo CEO wa zamani wa klabu hiyo David
Gill waliokuwa wakielekea kwenye mchezo wa klabu bingwa ya ulaya dhidi
ya Bayer Leverkusen, alisema kwamba tukio hilo lileta hali ya kutisha
miongoni mwa abiria huku akifhamika kwamba ilitolewa taarifa rasmi
kwamba kulikuwa na tatizo lilokuwa likiendelea.
Mlinzi
wa United Rio Ferdinand alitweet kuhusu tukio hilo muda mfupi baada ya
kutua salama akisema, 'Landed in Germany....just....I’ve only just
recovered after that choppy landing!
Kwenye
msafara huo hakuwemo Sir Bobby Charlton, mtu mmojawapo aliyenusurika
katika ajali iliyopita ya Munich, pia hakuwemo kocha mstaafu wa timu
hiyo Sir Alex Ferguson.
Pamoja
na kuchelewa kutua kwa ndege hiyo huko Cologne, Moyes na mlinzi Chris
Smalling walienda kwenye mkutano wa waandishi wa habari wakiwa watulivu
na wasiokuwa na chembe ya wasiwasi juu ya tukio hilo.
Usiku
wa leo United inacheza mechi muhimu na Leverkusen huku wakiwa wana
mapengo ya wachezaji wao muhimu kama Van Persie, Carrick, Jones na
Vidic.
MATOKEO YA JANA
Group E
Basel 1-0 Chelsea
Steaua Bucuresti 0-0 Schalke 04
Group F
Arsenal 2-0 Marseille
Borussia Dortmund 3-1 Napoli
0 comments:
Post a Comment