Saturday 23 November 2013

ARSENAL BADO YAENDELEA KUJIMARISHA JUU KILELENI POINTI 4 MBELE!

>>GIROUD APIGA 2 KUWAPAISHA ARSENAL, FULHAM, SUNDERLAND HALI TETE  WA CHAPWA 2 KILA MMOJA

BPL2013LOGOLIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Novemba 23
Everton 3 Liverpool 3
Arsenal 2 Southampton 0
Fulham 1 Swansea City 2
Hull City 0 Crystal Palace 1
Newcastle United 2 Norwich City 1
Stoke City 2 Sunderland 0
2030 West Ham United v Chelsea

ARSENAL 2 SOUTHAMPTON 0
Olivier Giroud ameifungia Arsenal Bao 2, moja kila Kipindi, naGIROUD Arsenal kujikita Pointi 4 mbele juu kileleni mwa Ligi Kuu England.
Arsenal walipata Bao la kwanza kutokana na zawadi murua toka Kipa wa Southampton, Artur Boruc, alipojidai ufundi baada kurudishiwa pasi na Giroud kumzidi maarifa na kufunga.
Baada ya zawadi hiyo, Arsenal walikosa Mabao baada Jack Wilshere na Aaron Ramsey kupiga posti na Nyota wa Southampton Adam Lallana na Jay Rodriguez kukosa kufunga Bao za wazi.
Giroud alifunga Bao la pili kwa Penati kufuatia Jose Fonte kumvuta Jezi Per Mertesacker.
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Koscielny, Mertesacker, Gibbs, Arteta, Ramsey, Wilshere, Ozil, Cazorla, Giroud. 
Southampton: Boruc, Clyne, Fonte, Hooiveld, Shaw, Wanyama, Schneiderlin, Ward-Prowse, Lallana, Rodriguez, Lambert.

FULHAM 1 SWANSEA CITY 2
Jonjo Shelvey alitoka Benchi na kuipa Swansea ushindi wao wa kwanza katika Mechi 6 na kuiacha Fulham ikihaha mkiani.
Swansea walitangulia kufunga kwa Bao la kwanza baada ya Aaron Hughes kujifunga mwenyewe lakini Scott Parker akaisawazishia Fulham.
Kipigo hiki cha Bao 2-1 Uwanjani kwao Craven Cottage kilifanya Mashabiki wa Fulham wapige kelele wakitaka Meneja Martin Jol atimuliwe.
VIKOSI:
Fulham: Stekelenburg, Zverotic, Hughes, Amorebieta, Richardson, Parker, Kasami, Boateng, Ruiz, Berbatov, Bent.
Swansea City: Vorm, Rangel, Chico, Williams (c), Davies, Canas, de Guzman, Dyer, Lamah, Pozuelo, Bony.

HULL CITY 0 CRYSTAL PALACE 1
Crystal Palace, ambao leo wamepata Meneja mpya Tony Pulis atakaeanza kazi rasmi Mechi ijayo, leo wameshinda Ugenini walipoifunga Hull City Bao 1-0 licha ya kuwa Mtu 10.
Yannick Bolasie alipewa Kadi Nyekundu kwa rafu dhidi ya Jake Livermore na muda mfupi baadae Barry Bannan akafunga Bao la ushindi.
VIKOSI:
Hull City: McGregor, Figueroa, Elmohamady, Davies, McShane, Huddlestone, Livermore, Boyd, Brady, Koren, Sagbo.
Crystal Palace: Speroni, Ward, Gabbidon, Delaney, Moxey, Jedinak, Dikgacoi, Bannan, Bolasie, Gayle, Chamakh.

NEWCASTLE UNITED 2 NORWICH CITY 1
Newcastle wamepata ushindi wao wa tatu mfululizo kwenye Ligi baada ya kuifunga Norwich City, inayoongozwa na Meneja wao wa zamani Chris Hughton,  Bao 2-1.
Newcastle walitangulia kufunga Bao 2 za Loic Remy na Yoan Gouffran huku Leroy Fer akiwapa Norwich Bao lao moja.
VIKOSI:
Newcastle: Krul; Yanga-Mbiwa, Coloccini, Williamson, Santon, Sissoko, Cabaye, Tiote, Gouffran, Shola Ameobi, Remy.
Norwich City: Ruddy; Martin, Turner, R Bennett, Olsson, Johnson, Fer, Howson, Redmond, Pilkington, Hooper 

STOKE CITY 2 SUNDERLAND 0
Stoke City wamepata ushindi wao wa kwanza katika Mechi 9 za Ligi katika hali tata baada ya kuifunga Mtu 10 Sunderland.
Stoke walifunga Bao lao la kwanza kupitia Charlie Adam lakini Sunderland walionewa sana pale Wes Brown alipopewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 36 kwa faulo ambayo hata hakumgusa Charlie Adam.
Bao la pili la Stoke lilifungwa na Steven Nzonzi.
VIKOSI:
Stoke City: Begovic; Cameron, Shawcross (c), Huth, Pieters; Walters, Nzonzi, Whelan, Adam, Arnautovic; Crouch.
Sunderland City: Mannone, Celustka, Bardsley, O'Shea, Brown, Ki, Colback, Larsson, Johnson, Giaccherini, Fletcher

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]

Jumapili 24 Novemba
1630 Manchester City v Tottenham Hotspur
1900 Cardiff City v Manchester United

Jumatatu 25 Novemba
2300 West Bromwich Albion v Aston Villa

LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Arsenal 12 14 28
2 Liverpool 12 11 24
3 Southampton 12 8 22
4 Chelsea 11 8 21
5 Everton 12 4 21
6 Man United 11 5 20
7 Tottenham 11 3 20
8 Newcastle 12 0 20
9 Man City 11 16 19
10 Swansea 12 1 15
11 West Brom 11 0 14
12 Aston Villa 11 -1 14
13 Hull 12 -6 14
14 Stoke 12 -2 13
15 Cardiff 11 -6 12
16 Norwich 12 -11 11
17 West Ham 11 -2 10
18 Fulham 12 -10 10
19 Crystal Palace 12 -14 7
20 Sunderland 12 -16 7

0 comments: